Na Jamiimojablogu, Mbeya
NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji ameitaka Mamlaka ya Mapato TRA Mkoa wa Mbeya kuhakikisha inaanda mpango maalumu kwa ajili kudhibiti mapato yanayopotea kutokana na kushamili kwa biashara ya ubadilishaji wa fedha kiholela katika mpaka wa Tunduma na Zambia.
Naibu waziri huyo ametoa kauli hiyo Mkoani Mbeya mara baada ya kutembelea Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoani humo na kutoa tathimini ya ziara yake aliyoifanya katika Mpaka wa
Tunduma na Zambia.
Tunduma na Zambia.
Amesema serikali imekuwa ikipoteza mapato mengi hasa kutokana na kuwepo kwa biashara
hiyo kiholela pasipo serikali kupata mapato yake hivyo ameitaka mamlaka hiyo kuhakikisha inaweka
mpango kabambe utakao iwezesha serikali kupata mapato yake kutokana na biashara
hiyo.
hiyo kiholela pasipo serikali kupata mapato yake hivyo ameitaka mamlaka hiyo kuhakikisha inaweka
mpango kabambe utakao iwezesha serikali kupata mapato yake kutokana na biashara
hiyo.
Amesema serikali lazima ijiendeshe yenyewe kwa kuongeza ukusanyaji wa mapato sanjali na
kuzuia mianya yote ya ukwepaji wa kodi pamoja na watu wote kuhakikisha wanalipa
kodi.
kuzuia mianya yote ya ukwepaji wa kodi pamoja na watu wote kuhakikisha wanalipa
kodi.
Amebainisha kuwa nchi inategemea mapato kwa ajili ya kutoa huduma muhimu kwa wananchi na hivyo kuwaongezea wananchi matumaini kwa kuwafikishia huduma muhimu.
Sehemu nyingine ambayo ameiagiza mamlaka hiyo kuishughulikia mara moja ili serikali iweze kupata mapato yake ni pamoja kuibuka kwa Saccos pamoja vikundi mbalimbali ambavyo vimekuwa
vikijihusisha na ukopeshaji wa fedha kwa liba kubwa hali ambayo pia imekuwa
ikiwapa mzigo mkubwa wananchi.
vikijihusisha na ukopeshaji wa fedha kwa liba kubwa hali ambayo pia imekuwa
ikiwapa mzigo mkubwa wananchi.
Katika hatua nyingine Naibu waziri huyo ameuagiza uongozi wa mamlaka ya mapato (TRA) Katika mpaka wa Tunduma na Zambia kuhakikisha kuwa mizigo yote inayosafilishwa kupitia mpaka huo inafanyiwa tathimini na kulipiwa kwa muda wa usio zidi siku moja tayari kuendelea na safari kwa inayoingia na kutoka nje ya Tanzania.
Ziara ya Naibu Waziri Dr. Kijaji ni ya kwanza Mkoani Mbeya tangu alipoteuliwa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania tarehe 11 Desemba 2015 kushika wadhifa huo.
Muungano wa Tanzania tarehe 11 Desemba 2015 kushika wadhifa huo.
Mwisho.