Naibu Waziri Fedha na Mipango Aomba Ushirikiano kwa Bodi na Uongozi TRA

Naibu Waziri wa Fedha akizungumza na Bodi ya Wakurugenzi pamoja na menejimenti ya TRA. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Bw. Benard Mchomvu na Kushoto kwake ni Naibu Kamishna Mkuu wa TRA, Bw. Lusekelo Mwaseba.

NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Ashatu Kijaji ametembelea Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili kufahamiana na Bodi ya Wakurugenzi pamoja na Uongozi wa TRA na kusisitiza msimamo wa serikali ya awamu ya tano katika suala zima la ukusanyaji wa mapato. Akizungumza wakati wa ziara yake katika ukumbi wa mikutano Makao Makuu ya TRA, Dr. Kijaji pamoja na kutoa pongezi kwa TRA kwa jukumu kubwa la kukusanya mapato, ameomba ushirikiano kutoka kwa Bodi na Uongozi wa TRA ili kuweza kuivusha Tanzania salama.

Ameongeza kuwa kuwepo ushirikiano kutasaidia TRA kuweza kufikia malengo ya serikali ya kukusanya kodi kwa ajili ya maendeleo ya taifa.

“Bila mapato hakuna taifa linalosonga mbele”, alisema Naibu Waziri ambaye aliambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dr. Servacius Likwelile.

Amesema nchi inategemea mapato kwa ajili ya kutoa huduma muhimu kwa wananchi na hivyo kuwaongezea wananchi matumaini kwa kuwafikishia huduma muhimu. Ameutaka uongozi wa TRA kushikamana na kuunga mkono kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya “Hapa Kazi Tu” kwa kusimama imara na kuwabaini wale wanaoichafua TRA na kuwachukulia hatua za kisheria. “Tusikubali wachache wanaotuchafua waendelee kutuchafua,” amesisitiza Naibu Waziri.

Dr. Kijaji amesema kwamba ili wafanyabaishara waifurahie TRA ni lazima kuimarisha ushirikiano kati yake na wafanyabiashara. Ili kuzidi kuongeza makusanyo, Naibu Waziri ameshauri kuwa misamaha itolewe kwa vigezo, kuimarisha makusanyo yatokanayo na madini. “Tukusanye kodi maeneo yote yanayostahili ili kupunguza utegemezi. Hakuna haja ya kupiga magoti kwa wahisani”, alisema Naibu Waziri na kuongeza kuwa serikali itaendelea kusimamia mazingira ya uchumi na kuhakikisha hakuna kodi ambazo zinakatisha tamaa wawekezaji.

Awali akimkaribisha Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TRA Bw. Benard Mchomvu amempongeza Naibu Waziri kwa niaba ya wafanyakazi wa TRA kwa kuchaguliwa kuwa Mbunge na hatimaye kuteuliwa na Rais kuwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango.

Naye Kaimu Kamishna Mkuu Dr. Philip Mpango amemweleza Naibu Waziri kwamba TRA ina wataalamu wazuri wa kodi na inakitumia vizuri Chuo cha Kodi kufundisha wafanyakazi ambao wengi wanakuwa wataalamu wa kodi. Amesema wafanyakazi wanaogundulika kukiuka taratibu za kazi wanachukuliwa hatua lakini wengine wanachapa kazi kwa kufanya jitihada za kukusanya mapato yanayoendana na uchumi wa nchi yetu. “Wafanyakazi wa TRA wanaipenda nchi yao”, amesema Kaimu Kamishna Mkuu.

Kuhusu kufikia lengo la makusanyo hadi Desemba mwaka huu, Dr. Mpango amesema anaimani idara zote za TRA zitafikia malengo. “Matarajio ni kujitahidi kukusanya na kufikia trilioni 1. 3 mwishoni mwa mwezi Desemba” alisema Naibu Kamishna Mkuu.
Ziara ya Naibu Waziri Dr. Kijaji ni ya kwanza tangu alipoteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 11 Desemba 2015 kushika wadhifa huo.

Imeandaliwa na Mkurugenzi Huduma na Elimu kwa Mlipakodi TRA