Naibu Waziri Chana Kufungua Mkutano Mkuu Baraza la Watoto

Watoto katika picha.

Watoto katika picha.


NAIBU Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Pindi H. Chana anatarajiwa kufungua Mkutano Mkuu wa Baraza la Watoto la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2014. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto leo kwa vyombo vya habari. Mkutano huo unatarajiwa kufanyika hapo kesho mkoani Morogoro katika ukumbi wa Chuo cha Walimu (CCT) kuanzia tarehe 11 hadi 12 Machi 2014.

Mkutano huo mkuu wa Baraza la Watoto utafanya kazi ya kupitia taarifa za utekelezaji za Mabaraza ya Watoto ya Wilaya na Mikoa Nchi nzima pamoja na kuchagua viongozi wapya wa Baraza hilo.