Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai akiwa na mkewe Dk. Fatuma akiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu, Luhama Chonya ambaye ni bibi mzaa mama, aliyemlea Naibu Spika. Mazishi hayo yalifanyika jana kijijini Ibwaga, wilayani Kongwa, Dodoma.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Luhama Chonya ambaye ni bibi mzaa mama wa Naibu Spika wa Bunge Ndugai, katika mazishi yaliyofanyika jana kijijini Ibwaga, wilayani Kongwa, Dodoma. (PICHA ZOTE NA MAGRETH KINABO – MAELEZO)