TANGAZO LA AJIRA JESHI LA POLISI – 2014/2015
Katika mwaka wa fedha 2014/2015 Jeshi la Polisi Tanzania linatarajia kuajiri wahitimu wa vyuo vya Elimu ya Juu wa mwaka 2013/2014. Ili kutekeleza azma hii waombaji watajaza kikamilifu na wataambatanisha vivuli vya vyeti vyao na kutuma Makao Makuu ya Polisi kwa njia ya Posta kabla ya tarehe 31.08.2014 kwa anuani ifuatayo:
Inspekta Jenerali wa Polisi,
Makao Makuu ya Polisi,
S. L. P. 9141,
DAR ES SALAAM
Waombaji wawe na taaluma zifuatazo:
Shahada: Menejimenti ya Rasilimali Watu, Utawala katika Utumishi wa Umma, Uchumi, Saikolojia na Ushauri Nasihi, Usimamizi wa Sheria na Utekelezaji[BaLE], Sheria, Ualimu, Maendeleo ya Jamii, Uandishi wa Habari, Uandishi wa Habari za Michezo, Mawasiliano ya Umma, TV & Redio Production, Michezo, Ugavi[BA in Procurement & Supplies], Mawasiliano ya Redio[Bsc in Radio Communication], Mazingira[BA in Environmental Disaster Mgt], Uhandisi Mitambo, Uhandisi Madini[Mining Engineering], Uchoraji[BA in Fine Arts], Fedha na Benki[Finance & Banking], Daktari[Medical Doctor] na Daktari wa Meno[Dental Surgeon], Mkemia, Bailojia[Molecular Biology].
Stashahada: Utunzaji Kumbukumbu, Katibu Muhutasi[Personal Secretaries], Mawasiliano ya Redio, Matengenezo ya Kompyuta, Fax na Photocopy Machines, Mafundi Mitambo wa Meli, Mafundi Umeme wa Magari, Ugavi[Procurement & Supplies], TV na Video Production, Manahodha, Tabibu[Clinical Officer], Tabibu wa Meno[Dental Therapist], Mzoeza Viungo[Psysiotherapist/Occupational Therapist], Fundi Sanifu Mionzi[Radiographer] na Fundi Sanifu Macho[Optometrist].
Astashahada: Uzamiaji, Mpishi, Fundi Pikipiki, Fundi Ushonaji na Muuguzi Msaidizi[Enrolled Nurse].
MASHARTI KWA MWOMBAJI
1. Mwombaji atajaza fomu ya maombi kikamilifu na atabandika
picha yake “Ppt Size” kwenye fomu.
2. Mwombaji aambatanishe katika fomu vivuli vya vyeti vyote
yaani cheti cha kuzaliwa, kuhitimu elimu ya sekondari[Leaving
& Academic], cheti/vyeti vya taaluma[Academic Transcript].
3. Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika.
SIFA ZA MWOMBAJI
1. Awe Mtanzania kwa kuzaliwa.
2. Awe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 25.
3. Awe amehitimu chuo mwaka wa masomo 2013/2014 tu.
4. Awe na tabia njema.
5. Asiwe na kumbukumbu za kutenda uhalifu.
6. Awe na afya njema[kimwili na kiakili]
7. Awe hajaoa/hajaolewa au kuwa na mtoto.
8. Asiwe na alama za kuchora mwilini[tatuu].
9. Awe na urefu usiopungua sentimita 155.
10. Asiwe mtumiaji wa madawa ya kulevya.
11. Awe hajaajiriwa na idara nyingine Serikalini.
12. Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya awali ya Polisi.
13. Awe tayari kufanya kazi popote ndani na nje ya Tanzania.