MFALME wa muziki wa taarab, Mzee Yusuf ametangaza kuachana rasmi na muziki huo na kuamua kumrudia mwenyezi Mungu.
Mzee Yusuf ametoa kauli hiyo leo Ijumaa ya Agosti 12, 2016 ikiwa ni muda mfupi baada ya kumaliza swala ya Ijumaa katika msikiti wa Ilala Bungoni jijini Dar es Salaam (Masjid Taqwa) huku akibubujikwa na machozi mengi.
Mzee Yusuf ameomba waumini wamuombee msamaha kwa Allah kwa kipindi chote alichokuwa amemuasi na kadhalika amewaomba wanamuziki wengine ambao ni waislamu kuachana na muziki na kuzitumia fani zao walizonazo katika kutangaza na kumsifia bwana Mtume Muhammad (s.a.w).
Hata hivyo amewaomba watu wote wenye CD za nyimbo zake majumbani pamoja na vituo vya redio na televisheni kuacha kupiga nyimbo zake na wakikaidi wafahamu madhambi yote yatakuwa juu yao kwani yeye hivi sasa anafanya toba Kwa Allah.