Na Mwandishi Wetu, Shinyanga
JESHI la Polisi Mkoa wa Shinyanga linamtafuta Daudi Giliama ambaye ni mzee wa umri wa miaka 60 kwa tuhuma za kumbaka mtoto wa miaka minne (4).
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Kamishina Msaidizi- ACP, Diwani Athumani amesema taarifa zinaeleza tukio hilo limetokea Kijiji cha Igutwa, wilayani Kahama.
Alisema mzee huyo anatuhumiwa kutenda kitendo hicho baada ya kumrubuni mtoto huyo na kumpeleka porini kisha kumtendea tukio hilo la kinyama lililomsababishia mtoto huyo maumivu makali mwilini.
Kamanda huyo amesema Giliama anadaiwa kukimbia kusiko julikana mara baada ya kufanya tukio hilo, hivyo Jeshi la Polisi mkoani hapa linamtafuta ili kumfikisha katika vyombo vya sheria kujibu tuhuma hizo.