Fundi Fudi maarufu kama Mzee Kipara amefariki dunia eneo la Kigogo jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa taarifa ambazo tumezipata kutoka kwa watu wa karibu wa Mzee Kipara, ni kwamba sasa ndugu jamaa na marafiki wanajiandaa kupeleka mwili wake Hospitali ya Mwananyamala kuuhifadhi. Mazishi yake yanatarajiwa kufanyika kesho, kwa taarifa zaidi tutawaletea hapo baadaye.