![Ndugu, jamaa na marafiki wakiuaga mwili wa mareheme Rhode Philipo Muze kabla ya kuanza safari ya kuelekea Usangi.](http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2012/05/DSC06416.jpg)
Ndugu, jamaa na marafiki wakiuaga mwili wa mareheme Rhode Philipo Muze kabla ya kuanza safari ya kuelekea Usangi.
![Wachungaji wakiongoza ibada ya kumuombea mareheme Rhode Philipo Muze kabla ya kuanza kwa safari kuelekea Usangi.](http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2012/05/DSC06380.jpg)
Wachungaji wakiongoza ibada ya kumuombea mareheme Rhode Philipo Muze kabla ya kuanza kwa safari kuelekea Usangi.
![Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Rhode Philipo Muze wakiutoa nje mwili tayari kwa kuanza kwa ibada.](http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2012/05/DSC06371.jpg)
Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Rhode Philipo Muze wakiutoa nje mwili tayari kwa kuanza kwa ibada.
MWILI wa marehemu Rhode Philipo Muze umesafirishwa jana kuelekea Usangi Mwanga mkoani Kilimanjaro tayari kwa mazishi yatakayofanyika Ijumaa ya Mai 12, 2012 saa tisa kijijini Usangi nyumbani kwa marehemu.
Ibada ya kumuaga marehemu Rhode Muze ilifanyika jana Kibaha Mwendapole nyumbani kwa dada wa marehemu, Mrs Kaiza na kuhudhuriwa na ndugu, jamaa na marafikia-ambao pia walitoa heshima za mwisho kabla ya mwili huo kusafirishwa kuelekea mkoani Kilimanjaro.
Marehemu Rhode Muze alifariki dunia Mai 7, 2012 Kibaha Mwendapole kwa ugonjwa wa kisukari ambao ulikuwa ukimsumbua kwa muda, ambapo amekuwa akitibiwa mara kadhaa katika hospitali za mikoa ya Dar es Salaam, Kilimanjaro na Pwani kabla ya mauti kumkuta. Marehemu alizaliwa Machi 26, 1934.