Mwili wa Dk. William Mgimwa Waagwa Dar

Rais Jakaya Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete, wakitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha, marehemu Dkt. William Mgimwa, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo mchana. Mwili huo umesafirishwa leo kuelekea Mkoani Iringa kwa maziko. Picha na OMR

Na Mwandishi Wetu

RAIS wa Tanzania leo ameongoza mamia ya wananchi na viongozi mbalimbali kutoa heshima za mwisho jijini Dar es Salaam kwa aliyekuwa Waziri wa Fedha Dk. William Mgimwa.

Shughuli nzima ya utoaji heshima za mwisho kwa marehemu Dk Mgimwa zilifanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, na baadaye mwili huo ulisafirishwa kuelekea mkoani Iringa kwa maziko.

Majonzi vilio na sura za uzuni ndizo zilizokuwa zimetawala kwenye viwanja hivyo muda mfupi baada ya kuwasili mwili wa marehemu kutokea katika hospitali ya Lugalo ya jijini Dar es Salaam. Miongoni mwa viongozi wa juu wa Serikali walioshiriki shughuli za leo ni pamoja na Rais Kikwete na Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal ambao wote waliongozana na wake zao.

Wengine ni pamoja na Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda, mawaziri wa Tanzania, Wakuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Davis Mwamunyange (JWTZ) na Ernest Mangu (IGP), Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Mama Maria Nyerere na viongozi mbalimbali wa serikali na vyama vya siasa. Wengine ni wakuu wa idara anuai viongozi viongozi wa taasisi za umma na binafsi na baadhi ya wananchi mbalimbali wakazi wa jijini la Dar es Salaam.