Mwigulu Aomba Urais, Ataja Vipaumbele, Alibeba Zege…!

Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Lameck Nchemba akitangaza nia kugombea urais.

Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Lameck Nchemba akitangaza nia kugombea urais.

Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Lameck Nchemba akitangaza nia kugombea urais.

Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Lameck Nchemba akitangaza nia kugombea urais.

Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Lameck Nchemba akitangaza nia kugombea urais.

Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Lameck Nchemba akitangaza nia kugombea urais.

Mwigulu Lameck Nchemba pamoja na familia yake mke na watoto.

Mwigulu Lameck Nchemba pamoja na familia yake mke na watoto.


Na Joachim Mushi

KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Lameck Nchemba leo ametangaza nia ya kugombea urais wa Tanzania kupitia chama chake, huku akieleza vipaombele vyake endapo atafanikiwa kupewa ridhaa hiyo na chama na baadaye wananchi kwenye uchaguzi Mkuu Oktoba 2015. Mwigulu ambaye ni Naibu Waziri Wizara ya Fedha alionekana kujenga hoja juu ya vipaombele vyake ametoa kauli hiyo leo mjini Dodoma.

Kati ya mambo aliyoanza nayo Mwigulu katika hotuba yake alieleza waziwazi kuwa mara baada ya kushinda nafasi hiyo, ataapishiwa Dodoma na nipo Serikali yake itahamia katika Mkoa huo wa Dodoma na kuanza kufanya kazi. Alisema amejitathmini na kuona ana ari na dhamira ya kubeba ajenda ya Watanzania kuelekea kuunda Serikali ya awamu ya tano. “…Ninaenda kubeba ajenda ya Watanzania…nina uwezo na dhamira ya kubeba ajenda za Watanzania,” alisema.

“…Jambo la kwanza la msingi na la msingi na la msingi…ni kuitambua ajenda ya Watanzania. Na Watanzania watamuunga mkono mtu aliyebeba ajenda yao…nilipokuwa natahmini niligundua kwamba nayatambua mazingira yote ya Watanzania, umaskini mimi sijausoma kwenye vitabu…sijajifunza umasikini vitabuni, nimeujua kuanzia nazaliwa mpaka nikaishi na mpaka nikajua mbinu za kuwatoa Watanzania kwenye umasikini…” alisema Mwigulu Nchemba akitangaza nia yake.

Alisema hoja za baadhi ya watu kudai sifa ya kiongozi ni kukaa sana madarakani hazina msingi wowote kwani kukaa saana madarakani (serikalini) si kigezo cha kuwa kiongozi bora, wala kuwa kijana si kigezo cha uongozi na kuongeza kuwa mfumo wa kukaa sana madarakani kwa nchi za kiafrika ni sawa ba mtu aliyesahau kabisa shida za wananchi. “…mtu aliyekaa sana madarakani ni mtu aliyesahau shida saana za Watanzania…Kiongozi kama sokoine hakumbukwi kwa kuwa alikaa sana Serikalini bali vitendo na uadilifu wake akiwa kiongozi,” alisema akiutubia umati wa wageni waliohudhuria mkutano huo.

“…Binafsi nakwenda kupambana na umasikini kwa kuwa nautambua vizuri umasikini. Nimezaliwa kwenye umasikini nimekulia kwenye umasikini, nimeishi kwenye umasikini hivyo sijausoma vitabuni. Wakati naanza maisha nilipomaliza chuo kikuu mkewangu amefanya kazi ya umamantilie…na mimi pia nimebeba zege…,” alisema Nchemba.

Aidha akifafanua hoja zake alisema ili taifa lifanikiwe lazima kuwe na mabadiliko ya ulipaji kodi kwa kila muhusika na kodi zitozwe kulingana na stahili za kila mmoja, huku akipinga uwepo wa utitiri wa kodi bila huduma husika kutolewa. “…haiwezekani watu kutozwa kodi ambazo haziwasaidii moja kwa moja, watu wanatozwa kodi za zimamoto ilhali hata gari la zimamoto halipo eneo lao, wakulima nao wanautitiri wa kodi huku zingine hazina tija kwao, watu wanatozwa kodi za taka ilhali hakuna magari ya taka maeneo yao.

Aliongeza lazima kubadilika kutoka taifa la kutegemea walipa kodi watumishi na waajiriwa serikalini na kwingineko na wafanyabiashara ndogondogo ilhali wafanyabiashara wakubwa wakikwepa na kusamehewa kodi hizo badala ya uwepo usawa katika ulipaji na msamaha wa kodi hizo. Alisema endapo ataingia madarakani atahakikisha anasimamia na kuziba mwanya wa matumizi mabaya ya fedha na rasilimali za umma, na kulibadilisha taifa kwa baadhi ya watumishi kufanya kazi kwa mazoea bila ya malengo.

Hata hivyo alisema atahakikisha njia zinazoonekana kuwapatia kipato Watanzania zitaboreshwa zaidi ili kuwasaidia Watanzania na kusimamia tendo la kuzibadili changamoto za masoko nchini kwa wakulima na wafugaji kuwa fursa. Alisema atazitumia vizuri sekta binafsi na hata kwa ubia kuwaongezea uwezo ili kusaidia kuwepo kwa viwanda vya kutosha ambavyo vitatumia malighafi za wakulima na wafugaji kutengeneza bidhaa.

“…Kuifanya Tanzania kuingia kwenye ulimwengu wa viwanda, nchi ikiingia kwenye uchumi wa viwanda na tunaweza kufunga mkanda na kuamua kutumia bidhaa zetu baada ya kuwezesha sekta ya viwanda ili kujenga soko imara la ndani kabla ya kwenda nje itasaidia kupunguza changamoto za masoko kwa wakulima na wafugaji,” alisema.

Aidha alisema ataitangaza rushwa kama janga maalumu na kesi zake zitashughulikiwa kwa haraka, na atakae bainika kala rushwa au kafanya ubadhilifu atachukuliwa hatua kali, ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kazi, kufilisiwa na kufungwa, kwani kumekuwa na udhaifu katika kupambana na hali hii ya rushwa ndio maana kumekuwa na rushwa ndani ya rushwa, uchunguzi juu ya uchunguzi.

Mwigulu Lameck Nchemba ambaye amejivua nafasi ya unaibu Katibu Mkuu wa CCM, alizaliwa Januari 7, Mwaka 1975 eneo la Makunda, Wilaya ya Iramba nchini Tanzanian. Amepata elimu ya Sekondari katika Shule ya Sekondari Mazengo na baadaye kidato cha tano na sita katika Sekondari ya Ilboru Mkoani Arusha kabla ya kuendelea na masomo ya juu (Chuo Kikuu) CHuo Kikuu cha Dar es Salaam. Mwigulu kwa sasa ni Naibu Waziri Wizara ya Fedha, nafasi aliyoingia tangu Mwezi Januari 2014.