Mwenyekiti WAMA Akutana na Daktari Bingwa Magonjwa ya Watoto

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na Daktari Bingwa wa Watoto Jerome Paulson kutoka Marekani na Viongozi wa Chama cha Madaktari wa Watoto hapa Tanzania kwenye ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, tarehe 21.5.2013.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea zawadi ya picha kutoka kwa Daktari Bingwa wa watoto Jerome Paulson aliyeambatana na Mkewe pamoja na viongozi wa Chama cha Madaktari wa watoto hapa Tanzania (Paediatrc Association of Tanzania-PAT). Kutoka kushoto ni Dr. Augustino Masawe akifuatiwa na Rais wa Chama cha Madaktari wa watoto nchini (PAT) Dr. Rodrick Kisenge, Mrs Jerome na kwa nyuma ni Dk. Francis Furia,Mjumbe na Dr. Hadija Mwamtemi, Mwekahazina wa chama hicho.