Hali hiyo itapelekea kuendelea kutoondoka barabarani hadi hapo rais huyo atakaposema hatawania kiti cha urais kwa awamu hiyo ya tatu.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana, Mwenyekiti huyo alisema wanawataka viongozi wa nchi za afrika mashariki kumshawishi raisi huyo au kumlazimisha kuachana na maamuzi hayo ya kugombea madaraka ya urais kwa awamu ya tatu.
Pia kumtaka rais huyo kutoa silaha ambazo zimezagaa kwa wananchi hao, na kuandaliwa mazingira bora ya chaguzi na utendeke kwa hali ya kuwa wanasiasa wanakuwa huru na kuacha kuwindwa na kufungwa.
Hayo yamejiri baada ya rais huyo kutangaza nia ya kuwania kiti hicho kwa awamu ya tatu ambayo ni kinyume cha sheria ya katiba ya nchi hiyo.
“Hali hii inaleta kumbukumbu ya historia ya zamani kwani yalitokea kama haya ambapo kulipelekea machafuko, na kuuawa kwa wale wote ambao hawapo sambamba na maamuzi ya rais huyo,” alisema.
Alisema hali ya usalama nchini humo ni ndogo kwani silaha zimezagaa kwa wananchi, wanajeshi na mgambo ambapo inahatarisha hata usalama wa nchi zilizopakana na nchi ya Burundi.
“Katika kipindi cha miaka kumi, hakuna hata siku moja ambayo raisi Pierre Nkuruzinza kuandaa kikao rasmi baina yake na vyama vya kisiasa na badala yake huweka wawakilishi wake, hakuna hata ndugu zake ambao wamechangia kukataa muhula huo si halali anakuwa adui yake na wengine kufukuzwa kazi na kuwindwa hadi kuuawa,” alisema.
“Huu muhula wa tatu hauna faida na taifa letu na ndiyo maana tumenzisha vuguvugu ambapo hatutaacha hadi hapo atakapo sema ameachana na awamu hiyo ya tatu, kwani amepata ushauri kutoka sehemu mbalimbali kama muungano wa watu wa ulaya, Afrika yenyewe, nchi za jumuia ya Afrika mashariki lakini pia kwa maaskofu, hivi sasa anataka kuwa sababu na chanzo cha machafuko kwasababu raia wa burundi kwa uoga wamekimbia nchi yao,” alisema.
Aidha alimpongeza rais wa Jakaya Kikwete kukubali kuwakaribisha wananchi wa Burundi na kuwapatia hifadhi.