Mwanamuziki ‘John Walker’ Afariki Dunia…!

Mwanamuziki Michael Denis (John Walker)

Mwanamuziki Michael Denis (John Walker)

AKIZUNGUMZA kwa njia ya simu na mwandishi wa habari hizi kaka wa marehemu Omari Milay, alisema walipigiwa simu alfajiri ya leo na kujulishwa kuwa ndugu yake Michael Denis a.k.a John Walker amefariki katika hospitali ya Muhimbili, alipokuwa akipata matibabu ya ajali aliyopata siku ya jana.

Taarifa zinasema John Walker alipata ajali ya kugongwa na kitu kizito kwenye paji la uso, alipokuwa gereji maeneo ya Sinza jijini Dar es Salaam akitengeneza gari yake, ambapo kwa bahati mbaya mtungi wa gesi ulilipuka na moja ya vipande vya chuma chenye ncha kali kikamchoma kichwani.

Tarifa za awali za madaktari zilisema wanahofia kipande hiko kimefika mbali kiasi kwamba damu inamwagikia kwenye ubongo. Alisema kwa sasa mipango ya mazishi inafanya kwa wanafamilia kukutana kujadili na mara itakapokamilika watajulisha watu nini kinaendelea.

Msanii John Walker ambaye alikuwa kwenye kundi la Watukutu Family, alijipatia umaarufu kwa nyimbo zake za Sophia, baby gal na nyinginezo, ambazo aliziimba kwa mtindo wa ulevi.