
Mwanamke akitoka shambani huku akiwa na mzigo wa kuni kichwani. Picha hii imepigwa Kijiji cha Kirando, Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa.
MWANAMKE maeneo anuai amekuwa akikumbana na changamoto mbalimbali za maisha ya kila siku, lakini kwa kundi la wanawake vijijini changamoto hizi zimekuwa ni maradufu ukilinganisha na zile za wanawake wanaoishi mjini na wenye fursha mbalimbali. Zifuatazo ni baadhi ya changamoto hizi ambazo hukumbana nazo wanawake vijijini kwa makundi anuai katika matukio ya picha zilizopigwa na mwandishi wa dev.kisakuzi.com maeneo husika.

Wanawake nyumbani ndio watafutaji zaidi wa maji vijijini, pichani binti akikokota baskeli yenye mzigo wa ndoo nne za maji kuelekea nyumbani. Picha hii imepigwa Kijijini Kishapu mkoani Shinyanga.

Haijalishi umri wala kimo kwa akinamama majukumu lazima yatimizwe, mabinti wakiwajibika kisimani Kishapu.

Changamoto si kwa wanawake tu bali hata kwa mabinti, pichani ni binti akiteka maji kwa ajili ya matumizi ya familia Kijiji cha Mhunze, Kishapu, Shinyanga

Shida ya maji kwa baadhi ya vijiji vya Wilaya ya Kishapu huwapa changamoto hata akinamama ambao umri wao umekwenda kidogo. Pichani ni mmoja wa akinamama aliyekula chumvi nyingi akiteka maji kwenye kisima cha msimu.

Hili ni moja ya soko la mazao linalotumiwa na vijiji kadhaa vya Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro. Idadi kubwa ya wauzaji na wanunuzi wa soko hili ni akinamama kutoka vijiji hivyo.

Changamoto ya majukumu kwa akinamama vijijini haijalishi umri. Pichani ni Bibi akifanya maandalizi ya chakula jikoni kwake. Picha hii imepigwa kijijini Isoso Wilayani Kishapu, Shinyanga.