Mwanahabari Rachel Mwiligwa azikwa

Baadhi ya waombolezaji wakiushusha mwili wa marehemu Rechal Mwiligwa kaburini nyumbani kwao Goba leo jioni Dar es Salaam.

Baadhi ya waombolezaji wakifuatilia mazishi ya marehemu Rachol Mwiligwa yaliyofanyika nyumbani kwao Goba leo.

Kutoka kushoto ni mmiliki wa Blog ya Jamii, Muhidin Michuzi, Mhariri wa Gazeti la Bingwa, Grace Hoka wakiwa na baadhi ya waombolezaji kwenye mazishi ya mpiganaji Rachol Mwiligwa.

Baadhi ya waombolezaji wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Rechal Mwiligwa kabla ya kuzikwa nyumbani kwao Goba.

Kutoka kushoto wa pili na watatu ni Mama na Baba wa marehemu Rachol Mwiligwa wakiweka udongo katika kaburi la mpendwa wao. Wa kwanza kulia ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika akiweka udogo kwenye kaburi la Mwiligwa katika mazishi hayo.

Na Mwandishi Wetu

ALIYAKUWA Mhariri wa Michezo wa Gazeti la Mtanzania, Rachel Mwiligwa linalochapishwa na kampuni ya New Habari (2006) Ltd ya jijini Dar es Salaam amezikwa leo nyumbani kwao Goba nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Safari ya mazishi ya marehemu Mwiligwa ilianza majira ya asubuhi katika Kanisa la Anglikana la Ubungo ambapo ilifanyika misa ya kumuombea na baadaye ndugu, jamaa na marafiki kipata muda wa kutoa heshima za mwisho kabla ya mwili kuelekea nyumbani kwao Goba kwa mazishi.

Baada ya mwili kuwasili nyumbani kwao Goba ibada ya mazishi iliendelea na majirani wa familia pamoja na ndugu, jamaa na marafiki kupatiwa nafasi nyingine ya kutoa heshima za mwisho kwa marehemu kabla ya mazishi kufanyika.

Mamia ya waombolezaji wakiwemo wafanyakazi wa kampuni ya New Habari, wanahabari kutoka vyombo mbalimbali, wakiongozwa na Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika bila kujali hali ya hewa (mvua) iliyokuwa ikinyesha walilimiminika nyumbani kwao na marehemu kumsindikika mpiganaji huyo katika safari yake ya milele.

Marehemu Mwiligwa alifariki mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kuugua kwa muda mfupi, kabla ya kulazwa siku kadhaa Hospitali ya Mwananyamala. Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya mpiganaji na mwanahabari Rechal Mwiligwa.