Mwanahabari Lyassa Ataja Vipaumbele Vyake Uchaguzi TUCTA

Mgombea Urais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi, Dismas Lyassa (katikati) akitangaza vipaumbele vyake katika mahojiano na waandishi wa habari Jijini. Kulia ni wakili Jebra Kambole, kushoto ni Meneja Kampeni wake Khamis Tembo.

Mgombea Urais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi, Dismas Lyassa (katikati) akitangaza vipaumbele vyake katika mahojiano na waandishi wa habari Jijini. Kulia ni wakili Jebra Kambole, kushoto ni Meneja Kampeni wake Khamis Tembo.

Mgombea Urais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi, Dismas Lyassa (katikati) akitangaza vipaumbele vyake katika mahojiano na waandishi wa habari Jijini. Kulia ni wakili Jebra Kambole, kushoto ni Meneja Kampeni wake Khamis Tembo.

Mgombea Urais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi, Dismas Lyassa (katikati) akitangaza vipaumbele vyake katika mahojiano na waandishi wa habari Jijini. Kulia ni wakili Jebra Kambole, kushoto ni Meneja Kampeni wake Khamis Tembo.

MWANAHABARI mkongwe, Dismas Lyassa ambaye anagombea nafasi ya Urais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) leo amezungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam akitaja vipaumbele vyake endapo atafanikiwa kushinda katika nafasi hiyo. Lyassa ambaye kwa sasa ni Mhariri wa Biashara na Uchumi wa Gazeti la Mwananchi, alisema lengo lake kuu ni kuhakikisha anaifufua TUCTA kuwa hai na kuleta mabadiliko ya kweli kwa kuzingatia vipaumbele ambavyo ameviweka wazi mbele ya wanahabari.

Mwanahabari huyo mwenye takribani miaka 20 katika tasnia ya habari alisema kipaumbele cha kwanza atakapoingia madarakani ni kupigania na kulinda haki za wafanyakazi; lengo likiwa ni kuondoa matatizo sugu ya wafanyakazi.
Aliyataja baadhi ya matatizo hayo ni pamoja na kulipwa ujira/mishahara duni, ocheleweshaji wa upatikanaji wa ujira/mishahara, ucheleweshaji fedha za kujikimu kwa waajiriwa wapya na kiwango kidogo cha fedha za kujikimu, uhaba au kutokuwepo kabisa makazi kwa wafanyakazi wapya.

Matatizo mengine ni rushwa na kuajiri kwa misingi ya kujuana, wakubwa yaani mabosi kujifanya Mungu kwa kuwaendesha wafanyakazi kwa kadri wanavyotaka wao, ilhali sivyo inavyosema sheria na uwepo wa mpangilio usio sawa wa ujira na mishahara. Vipaumbele vingine alivyovitaja ni kushughulikia tatizo la ajira kuporwa na wageni, ingawa sheria na sera za ajira zinaeleza wazi kwamba hairuhusiwi wageni kuingia nchini zaidi ya watano kwa kazi ziziso na ujuzi.

Mgombea Urais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi, Dismas Lyassa akizungumza na waandishi wa habari Jijini akiwa na timu yake.

Mgombea Urais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi, Dismas Lyassa akizungumza na waandishi wa habari Jijini akiwa na timu yake.


“…Nitahakikisha wazawa wanapewa fursa ya kufanya kazi nchini; hii ni pamoja na kuomba CV za wageni ili tuone kama ni kweli hakuna Watanzania wenye sifa za kufanya hiyo kazi hiyo.

“…Kumekuwa na taarifa za uwepo wageni katika makampuni kadhaa yakiwamo mahoteli, migodi, viwanda vya sarufi n.k. ambao baadhi wanalipwa malipo makubwa tofauti na wazawa japo hawana elimu au ujuzi wa kuwazidi wazawa. Nitakuwa na kamati maalumu ya kufuatilia waajiriwa wote Tanzania hasa wageni ili kujua kama wanazo sifa za kufanya kazi au wanapora nafasi za Watanzania.”

Aidha alisema katika mabadiliko yake amepanga kuanzisha idara mbili mpya na kuboresha zilizoko kuhakikisha uwepo wa ufanisi zaidi kiutendaji na kuona TUCTA kwa kushirikiana na vyama shiriki vinashirikiana kuondoa changamoto anuai zinazolikabili shirikisho hilo. Alizitaja idara mpya atakazozianzisha ni Idara ya Walemavu itakayo angalia hali ya maisha ya wafanyakazi walemavu nchini ikiwamo kuwasaidia kupata baiskeli na huduma zingine muhimu.

Aliitaja idara ya pili ni Idara ya fursa ‘Career Development Department’ na Mafunzo ambayo itakuwa daraja la kuibua fursa zinazoendelea nje ya nchi na kuziunganisha na wafanyakazi nchini.

“…Nimetembea katika nchi tofauti Duniani ikiwemo Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Mauritius, India, Thailand, Sweden na Marekani…nimeona fursa kadhaa ambazo zimenishawishi kuanzisha idara maalum ya kusaidia wafanyakazi kufahamu fursa zinazoendelea Duniani na hapa nchini. Fursa hizo zitakuwa zinapatikana katika tovuti za TUCTA na ofisi za vyama vya wafanyakazi mikoani,” alisema.

“Baadhi ya fursa ni namna gani mtu anaweza kusoma nje ya nchi bila kulipa ada kwa kozi za muda mrefu na mfupi, fursa ya mashirika ambayo yanatoa misaada kwenye sekta mbalimbali. Kwa mfano kuna mashirika kama www.nuffic.nl au vyuo ambavyo mtu anaweza kusoma bure bila kulipa chembe ya ada kama www.berea.edu ya Marekani na fursa nyingine nyingi. Nimegundua Watanzania wengi hawanufaiki sana na fursa hizi. Ziko pia taasisi nyingine zinatoa,” alisema mgombea huyo urais wa TUCTA.

Akifafanua zaidi aliongeza kuwa idara hiyo itakuwa na majukumu ya kutoa elimu kwa wafanyakazi kuzifahamu sheria za kazi, hali kadhalika itakuwa inawasiliana na waajiri ili zaidi ya barua ya ajira au mkataba wanaompa mwajiriwa, ampe pia na chapisho letu ambalo mwajiriwa anapaswa kupewa siku ya kuajiriwa kwake ili ajue kwa uhakika sheria za kazi zinasemaje…,” alisema.

Mambo mengine ambayo Lyassa amepanga kuyafanya atakapofanikiwa kuingia madarakani ni pamoja na kulifufua gazeti la Mfanyakazi ndani ya siku 90 ili liwe sauti thabiti ya wafanyakazi kazi ambayo ameahidi kuifanya kwa hali na mali.

“…Haijalishi kama TUCTA itakuwa na fedha au la, nitahakikisha ndani ya siku 126 litakuwa mitaani likiandika habari mbalimbali hasa likitumika kama sauti ya wafanyakazi na yote ambayo yataonekana ni ya maana kwa ustawi wa taifa. Nina uzoefu zaidi ya miaka 20 katika sekya ya habari kama Mhariri, na hata sasa ni Mhariri wa Biashara gazeti la Mwananchi, nitahakikisha tunatafuta fedha ndani na nje ya TUCTA ikiwamo kuwatumia wafanyabiashara kwa kubadilishana msaada kwa matangazo kwa muda, ili hatimaye liweze kuwa mitaani. Ni aibu kubwa kuona nchi ina wafanyakazi wengi, lakini gazeti kama hili la wafanyakazi haliko mitaani,” alisema Lyassa.

Katika mkutano na wanahabari mgombea huyo aliambatana na mke Mchungaji Rightess Lyassa wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Kawe -Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Mawasiliano na Usafirishaji (COTWU) kanda ya Dar es Salaam, Mussa Mwakalinga, wakili wake Jebra Kambole kutoka kampuni ya Law Guards ya Jijini Dar es Salaam, na Meneja kampeni wake Khamis Tembo.