Agnes aliokotwa na msamaria mmoja ambaye kwa taarifa za awali zinasema alikuwa ni mlinzi wa nyumba moja maeneo ya Koko Beach ambako ndio alikutwa ametupwa na watu wasiofahamika na kupelekwa kituo cha Polisi cha Oysterbay na baadae kukimbizwa hospitali ya Agha khan.
Marehemu Agnes B. King’unza alifariki Jioni ya tarehe 16/07/2012 katika Hospitali ya Muhimbili ambako alipelekwa baada ya Madaktari wa Hospitali ya Agha khan kushindwa kumtibu na kumrufaa Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Mwili wa Marehemu Agnes King’unza umesafirishwa kwenda Nyumbani kwao Kalenga – Iringa kwa mazishi ambayo yatafanyika 19/07/2012.
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.