Mwalimu Nyerere Ataendelea Kuwa Baba wa Taifa Milele…!

Mwalimu Julias Kambarage Nyerere

Mwalimu Julias Kambarage Nyerere

LEO ni kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julias Kambarage Nyerere. Kila ifikapo Oktoba 14 kila mwaka Tanzania inaadhimisha kumbukumbu ya kifo cha Rais huyu wa Kwanza wa Tanzania aliyepewa sifa ya kuwa baba wa taifa kutokana na mambo mengi ya msingi aliyojitolea kwa taifa hili.

Leo hii ni miaka 13 imepita tangu Mwalimu Nyerere alipofariki dunia. Julius Kambarage Nyerere alizaliwa mwaka 1922 katika Kijiji cha Butiama, wilaya ya Musoma, Mkoa wa Mara, Tanzania (wakati ule ikiitwa Tanganyika). Nyerere ni mmojawapo kati ya watoto 26 wa Nyerere Burito, aliyekuwa chifu wa kabila la Wazanaki.

Kwa kifupi twaweza kusema kuwa Mwalimu Nyerere ni kiongozi wa kwanza aliyelitoa taifa letu katika minyororo ya wakoloni na ndio maaana alipewa heshima ya kuwa ‘Baba wa Taifa’. Hata hivyo kiongozi huyu aliendelea kulipigania taifa hata baada ya uhuru wa huku akifanya harakati za kuhakikisha ukomozi kwa nchi nyingine za Afrika. Hizi ni miongoni mwa sifa kedekede alizojijengea kiongozi huyu.

Kwa kutambua hayo mtandao wa dev.kisakuzi.com- www.thehabari.com unawatakia Watanzania wote kumbukizi njema ya maadhimisho mema ya kiongozi huyu mahiri wa nchi na Afrika kwa ujumla.