Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro (kushoto) wakizindua rasmi vyoo ilivyojengwa katika shule za msingi 10 wilayani Moshi za kufadhiliwa na UNDP.

Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini ,Alvaro Rodriguez
wakiwa katika picha za pamoja na wanafunzi wa shule za Azimio na Mandela.
MWAKILISHI wa Shirika la Mipango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez, akishirikiana na Mkuu wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Balozi Celestine Mushy wamezindua vyoo 10 vilivyojengwa katika shule za msingi 10 wilayani Moshi.
Afrika Mashariki, Balozi Celestine Mushy wamezindua vyoo 10 vilivyojengwa katika shule za msingi 10 wilayani Moshi.
Ujenzi huo ulifanyika ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya uwapo wa Umoja wa Mataifa. Wakati wa maadhimisho hayo pia wafanyakazi wa Umoja wa
Mataifa walifanya shughuli mbalimbali mkoani Kilimanjaro za kusaidia maendeleo ikiwamo hifadhi ya mazingira na usafi.
Mataifa walifanya shughuli mbalimbali mkoani Kilimanjaro za kusaidia maendeleo ikiwamo hifadhi ya mazingira na usafi.
Katika kuhakikisha kwamba shule zinakuwa na UNDP Tanzania ilisaidia mkoa wa Kilimanjaro Sh Mil 510 kujenga vyoo vya kisasa katika shule za msingi 10 ili kusaidia kuezesha usafi kwa wanafunzi na walimu wao.
Hadi kufikia sasa jumla ya matundu 178 yamejengwa katika shule 10 ambapo matundu 104 ni kwa ajili ya wasichana na 74 kwa ajili ya wavulana.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mwakilishi makzi wa UNDP, Alvaro Rodriguez alipongeza mradi huo na ushirikiano uliokuwepo kati ya serikali, wao na shule ikiwa ni hatua moja ya maendeleo endelevu kwa kuboresha mazingira ya usafi kwa wanafunzi wa kike na wa kiume katika masomo yao na hivyo kuimarisha safari ya kuelekea malengo ya dunia ya 2030.
Alisema kutokuwepo kwa mazingirabora ya usafi ni chanagamoto
kubwa kwa wanafunzi na hali hiyo inawaathiri sana wanafunzi wa kike.
kubwa kwa wanafunzi na hali hiyo inawaathiri sana wanafunzi wa kike.
Rodriguez alisema kutokana na kujengwa kwa vyoo hivyo wanafunzi ,walimu na walezi sasa watakuwa na kazi pekee ya kuhakikisha kwamba wanatoa elimu bora .
“Watoto wa kike watakuwa na changamoto chache zaidi za mahudhurio shuleni na wakati huo huo masuala ya usafi yatakuwa yameboreka na hivyo kuwa na wanafunzi na familia zenye siha njema.”alisema Rodriguez.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa
katika wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki ,Balozi
Celestine Mushy amepongeza kwa msaada huo na kuutaka Umja wa Mataifa kuendelea kutoa msaada kwa shule zenye mahitaji makubwa kuhakikisha kwamba malengo ya dunia yanayohusiaa na usafi ,mazingira na maji safi yanafanikiwa ifikapo mwaka 2030.

Naye mkuu wa wilaya ya Moshi, Kippi Warioba pamoja na kuishukuru UNDP kwa kazi nzuri waliyofanya pia alizitaka jumuiya za maeneo yaliyojengewa vyoo kuiliki msaada huo kwa kuhakikisha wanaitumia na hivyo kuisadia kufikia malengo ya dunia 2010.