Mvua Zaleta Mafuriko Maeneo ya Vijijini Mkoani Kilimanjaro

Mbunge wa viti maalumu ,Lucy Owenya (Chadema) (kulia)akiwa ameongozana na diwani wa kata ya Arusha Chini ,Rojas Mmari alipotembelea kujionea athari zilizotokana na mafuriko hayo.

Mbunge wa viti maalumu ,Lucy Owenya
(Chadema) (kulia)akiwa ameongozana na diwani wa kata ya Arusha Chini
,Rojas Mmari alipotembelea kujionea athari zilizotokana na mafuriko
hayo.

Mafuriko makubwa yamevikumba vijiji saba
kikiwemo kiwanda cha sukari cha TPC na kuathiri miundombinu pamoja na
makazi ya watu kujaa maji.
Mbunge Lucy Owenya akitembelea maeneo yaliyo
athirika na mafuriko hayo.
Mbunge Lucy Owenya akitizama sehemu ambayo
wananchi walilazimika kuibomoa kwa kushirikiana na uongozi wa kiwanda
cha TPC ili kuruhusu maji kupita.
Eneo lililobomolewa ili kuruhusu maji ya
mafuriko kupita.
Baadhi ya nyumba zilijaa maji hali
iliyowalazimu wahusika kutoa itu vya ndani nje.
Wengine walilazimika kuweka vyakula juu ya
mabanda ya kuku.
Baada ya maji kujaa wengine walilazimika
kuhamishia magodoro yao juu ya paa la Choo.
Hata vyakula ambavyo vingi vyao vililowa na
maji vilianikwa juu ya paa.
Mbunge Lucy Owenya akitizama namna ambavyo
baadhi ya wananchi walivyoamua kuokoa vitu ya kwa kuianika juu ya
paa.
Mifugo pia liathirika na mafuriko
hayo.
Kutokana na hali hiyo Mbunge Lucy Owenya
alilazimika kutoa msaada wa chakula kwa waathirika wa mafuriko
hayo
Mbunge Lucy Owenya akimfariji mmoja ya
waathirika wa mafuriko hayo aliyekuwa akilia kwa uchungu baada ya
kupoteza vitu vyake mbali,mbali ikiwemo vyeti vya taaluma ya
utabibu.
Mbunge Lucy Owenya akikabidhi msaada wa
chakula kwa wananchi walioathirika na mafuriko hayo.
Mbunge Lucy Owenya akizungumza mara baada ya
kukabidhi msaada huo.
Diwani wa kata ya Arusha Chini Rojas Mmari
akizungumza jambo mara baada ya wananchi wake kukabidhiwa msaada
huo.
Afisa mtendaji Utawala wa kiwanda cha sukari
cha TPC ,Jafary Ally akizungumza kuhusu namna mafuriko hayo yalivyo
athiri kiwanda hicho.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii
Kanda ya Kaskazini