Hiki ni kivuko muhimu sana katika mustakabali mzima wa kuwaunganisha wakazi wa Kigamboni, ambao wapo kisiwani na wale wa mjini, yaani nchi kavu. Wakazi wa kigamboni huita mjini “Ng’ambo” na wengi hutumia kivuko hiki kila siku kwa ajili ya kwenda ng’ambo kufanya shughuli zao za kila siku.