Na Biseko Lisso Ibrahim, WUUM (U)
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya uchukuzi), Eng. Dkt. Leonard Chamuriho ameipongeza kampuni ya huduma za meli nchini (MSCL), kwa kukarabati meli zake kwa kutumia fedha za ndani na hivyo kuhuisha utendaji kazi wa kampuni hiyo.
Akizungumza jijini Mwanza mara baada ya kukagua huduma zinazotolewa na kampuni hiyo Eng. Dkt. Chamuriho amesema Serikali itawekeza kikamilifu kwenye kampuni hiyo baada ya kuridhika na utendaji uliopo sasa.
“Fanyeni kazi kwa bidii na fikra mpya Serikali inashughulikia kwa karibu suala la mishahara yenu na stahili nyingine” amesema Eng. Dkt. Chamuriho.
Hivi karibuni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa alimteua Kaimu Meneja Mkuu mpya wa kampuni hiyo Bw. Eric Hamisi ambaye kwa kushirikiana vema na menejimenti na wafanyakazi wamewezesha kuongeza mapato kwa kwa asilimia 100.
Kampuni ya huduma za Meli MSCL ni moja ya kampuni ya Meli yanayomilikiwa na Serikali kwa asilimia 100 na kusimamiwa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Sekta ya Uchukuzi na inatoa huduma za usafirishaji wa abiria na mizigo katika maziwa makuu yaliyopo nchini Victoria,Nyasa na Tanganyika