MUVI yang’ara Maonesho ya Wajasiriamali

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Cyril Chami pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dk. Christine Ishengoma wakiwa katika Banda la MUVI. Wengine ni maofisa wawili wa MUVI, Bi. Nema Munisi na Dunstan Mhilu wakitoa maelezo kwa viongozi hao.

Na Dunstan Mhilu

MUUNGANISHO wa Ujasiriamali Vijijini (MUVI) umefanikiwa kufanya vizuri katika Maonesho ya wajasiriamali wadogo na wakati Kanda ya Kusini yaliyokuwa yakifanyika hivi karibuni wilayani Mbinga, kwenye viwanja vya CCM. Banda la MUVI lilionekana kusheheni kila aina ya vipeperushi vilivyokuwa vimeandaliwa kwa ajili yakutoa elimu kwa wajasiriamali hususani wa zao la muhogo na alizeti waishio Mkoa wa Ruvuma.

Vipeperushi vilionekana kuvutia wengi kutokana na kile kuandaliwa kwa lugha nyepesi ya Kiswahili ili kufikisha ujumbe kwa wakulima. Lengo kubwa la ujumbe katika vipeperushi ni kuongeza thamani ya bidhaa zitokanazo na mhogo pamoja na alizeti. 

Bi. Nema Munisi ni Mratibu wa Mradi huo Mkoa wa Ruvuma, akitoa elemu kwa watu kada mbalimbali anasema lengo la MUVI ni kuhakikisha maisha ya Mtanzania hasa wa kijijini yanaboreshwa kupitia ujasiriamali ambao umejikita katika soko la bidhaa za muhogo na alizeti.

“Tunapozungumzia mnyororo wa thamani tuna manisha kuunganisha nguvu kazi kwa wataalamu mbali mbali walio bobea katika fani mbalimbali wakiwemo maofisa ugani, maofisa habari, biashara n.k kutoka kwa mzalishaji, mnunuzi na mlaji hi ndiyo shabaha ya MUVI ikiwemo kuwajengea uwezo nakuwapatia mafunzo anuai ya uzalishaji bora na uandaaji wa bidhaa bora zenye kuhimili changamoto za soko ndani na nje ya Tanzania.”

Naye Ofisa Habari wa mradi huo Mkoa wa Ruvuma Bw. Dunstan Mhilu anasema wamejiandaa vya kutosha kwani walijua bila kufanya hivyo elimu ya kutosha kwa wajasiriamali na wale wasiyo wajasiriamali itakuwa ni kutowatendea haki.

“Ndiyo maana tumejipanga na si kujipanga kwa ajili ya maonesho lahasha utendaji kazi kwa bidii ni silika ya wana MUVI popote walipo kuanzia ngazi ya wana vikundi hadi maafisa wa mradi huo.” Anasema.

Kulia ni Ofisa Biashara na Ufundi wa SIDO Mkoani Mbeya, Bw Japhet, Ofisa Biashara Bw. David Mng'ongo African Image, Ofisa biashara SIDO Ruvuma Bw. Seleman Madamba, Bw. Salum Lupande Mratibu wa Muvi toka PWC na Bi. Nema Munisi Mratibu MUVI, Ruvuma(Picha zote na Dunstan Mhilu)


Bw. Dunstan aliongeza kusema, “Ki msingi tunapenda kutumia njia rahisi katka mawasiliano ili kukidhi matakwa na viwango vya mawasiliano kwa hadhira iliyo kusudiwa, ndiyo mana vipeprushi vimejaa lugha ya picha vikielezea dhana ya mnyororo wa thamani. Kama hiyo haitoshi tume wawekea luninga ili waweze kuona kile ambacho wana MUVI wanafanya kutoka maeneo mbali mbali ya mkoa wa Ruvuma ni ukweli usio pingika watu walifurika katika banda la MUVI si kwa lengo la kushangaa bali kujifunza mambo mbali mbali kutoka kwa maafisa waliyokuwepo katika banda la MUVI.”

Kutoka kushoto ni Ofisa Habari wa Mradi wa MUVI, Bw. Dunstan Mhilu akifuatiwa na Muandaaji na Muendesha vipindi vya redio katika mradi wa MUVI, Bw. Mark na mwisho ni Ofisa Biashara wa mradi wa MUVI kutoka African Image Production Ltd, Bw. David Mng'ongo


Maonesho hayo yamefikia kilele chake huku mkuu wa wilaya ya mbinga akiwaasa Sido kutokuwaacha wajasirimali wa mkoa wa Ruvuma na kusini kwa ujumla ikiwemo kuwapatia uelewa, kupanua vipaji, kupanua wigo wa uendelezaji wa teknolojia na kuhamasisha ubora wa bidhaa zinazo zalishwa na wajasiriamali wadogo na wale wakati.