MSANII moja toka Uingereza amekamatwa nchini Uganda kwa madai ya kuandaa na kuonesha mchezo wa kuigiza kuhusu ushuga. Taarifa kutoka Uganda zinasema Muingereza huyo alionesha mchezo huo wa kuigiza licha ya kwamba Uganda ilipiga marufuku kwa muda onesho hilo.
Mtayarishi David Cecil wa Uingereza alifikishwa katika mahakama moja mjini Kampala na kushitakiwa kwa madia ya kukaidi na kupuuza amri ya Serikali. Mahakama hiyo iliambiwa kuwa Bwana Cecil alionyesha mchezo huo kwa jina “The river and the mountain” katika ukumbi wa Tilapia Cultural Center tarehe 17 Agosti na pia katika ukumbi mwengine wa Mish Mash Cultural Center tarehe 26 Agosti mjini Kampala.
Mahakama hiyo ya Kampala ilikataa kuamuachilia Muingereza huyo kwa dhamana na badala yake kuagiza awekwe katika gereza la Luzira hadi siku ya Jumatatu, Septemba 17 ambapo kesi yake inatarajiwa kuendelea.
-BBC