FAMILIA ya Ankal Issa Michuzi iliyopatwa na msiba wa kuondokewa na Mtoto wa Ankal, Maggid Muhidin aliefariki Jumapili Mei 8, 2016 huko Durban, Afrika Kusini.
Mwili wa marehemu unatarajiwa kuwasili nchini kesho Ijumaa Mei 13, 2016 mnamo majira ya saa saba mchana na ndege ya shirika la Emirates (hiyo ni kutokana na kukosekana kwa nafasi katika ndege za moja kwa moja kuja nchini), hivyo kwa wale watakaojaaliwa kwenda kuupokea mwili wa kijana wetu, wafike pale uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere, Jijini Dar es salaam hiyo kesho kuupokea.
mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi saa kumi alasili katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam, na taratibu zote za kuandaa mazishi zitaanza kufanyika kuanzia saa nne asubuhi siku hiyo ya jumamosi, nyumbani Tegeta.
Msiba uko Tegeta Wazo Hill, Nyumbani kwa Mama Mzazi wa Marehemu (likiwa ni ombi maalum la Mama).
NAMNA YA KUFIKA MSIBANI
Ukitokea Tegeta Kibaoni kama unaelekea Kiwanda cha Cement Wazo, mbele mkono wako wa kulia utaona Kanisa la KKKT na ukienda mbele tena kidogo, utaona uzio wenye rangi ya njano umeandikwa Twiga Cement, unakatisha hapo upande huo huo wa kulia. ukikatisha tu utaona kuna mtaa mwingine unaingia upande wa kulia, uache na usogee mbele, utaona mtaa mwingine unaingia kulia, ingia nao huo na utakuwa umefika msibani.
Innalillah wa inna ilayhi raajiun
-AMIN.