MTU mmoja mmwenye umri kati ya 65-70 ameuawa baada ya kupigwa na Rungu kichwani na mtu anayedaiwa kuwa ni mtoto wake, Mkazi wa Wilaya ya Rombo, Mkoani Kilimanjaro. Ofisa Mtendaji wa Kijiji Cha Ikuini, Gaspar Kauki amekiri kutokea kwa tukio hilo na kwamba limetokea mnamo Agosti 8, mwaka huu majira ya saa nne usiku katika kitongoji cha Imongoni Kijiji cha Ikuini.
Pia amemtaja aliyeuawa kuwa ni Onesphori Shirima na anayetuhumiwa kuhusika na mauajai hayo ni mtoto wake anayefahamika kwa jina la Christogoni Shirima maarufu kama SINGERE (40) mkulima na mkazi wa kijiji cha ikuini.
Kauki amesema kuwa chanzo cha mauaji hayo kimetokna na ugomvi kati ya marehemu na mwanae ambapo imedaiwa kuwa walikua na ugomvi wa muda mrefu na kwa siku hiyo ya jana walikua na ugomvi mkubwa kati yao na hivo wakati ugomvi huo ukiendelea ndipo mtuhumiwa alichukua rungu na kumpiga kichwani na kupelekea kifo.
Mtuhumiwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi na mwili wa Marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Huruma wilayani Rombo. Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.