Mtoto Auwawa, Akatwa Ulimi, Sehemu za Siri na Kulawitiwa

Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi, Ernest Mangu.

Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi, Ernest Mangu.


Na Mwandishi Wetu, Moshi

WATU watatu wamefariki dunia mkoani Kilimanjaro katika amtukia matatu tofauti likiwama la mtoto wa darasa la nne kuuwaa kinyama kwa kukatwa sehemu za siri na ulimi pamoja na kulawitiwa.

Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Flugence Ngonyani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai limetokea Mai 23, 2015 majira ya saa 1:00 asubuhi katika Kijiji cha Katanini Kata ya Karanga Manispaa ya Moshi.

Ngonyani alisema mtoto Fraterin Massawe (11) mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi magereza aliokotwa akiwa ametupwa katika shamba linalomilikiwa na masista wa kanisa katoliki lililopo karanga.

Amesema mtoto huyo alikutwa akiwa na jeraha kubwa usoni, huku korodani zikiwa zimeondolewa pamoja na ulimi na kwamba anaonekana kulawitiwa kutokana na kukutwa na haja kubwa. Taarifa za awali zinasema mtoto huyo alitoweka nyumbani may 21 mwaka huu na kwamba alionekana na mtu alitajwa kuwa ni Mariki Peter Olomi(45) mkazi wa Kibosho road.

Kamanda alisema mtuhumiawa anashikili kwa uchunguzi zaidi na kwamba mwili wa mtoto huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa ya mawenzi. Katika tukio lingeni mtoto mwenye umri wa miaka miwili ameokotwa akiwa amekufua katika dimbwi la mto makombero ulioko kijiji cha kikelelwa wilayani Rombo.

Kamanda Ngonyani, alisema tukio hilo lilitokea Mai 24, 2015 saa 8:30 asubuhi ambapo mtoto Daud Method alikutwa akielea katika dimbwi hilo na kwamba chanzo cha kifo bado hakijajulikana. Tukio lingine lilitokea Mai 24 mwaka huu, saa 3:30 asubuhi maeneo ya Marangu pentekote mtembea kwa miguu alidongwa na gari na kupoteza maisha papo hapo.

Kamanda amemtaja kuwa ni Dismas Lyamuya (45) aligongwa na gari aina ya fuso yenye namba za usajili T941 CQS,lililokuwa likiendeshwa na Abdulla Muhamed (39) na kwamba dereva anashikiliwa kwa kosa la kuacha njia na kwenda kumgonga mtembea kwamiguu.