MTIHANI WA UWAKALA WA FIFA IJUMAA


Logo ya FIFA

MTIHANI wa Uwakala wa Wachezaji wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu
(FIFA) utafanyika Septemba 29 mwaka huu. Mtihani huo utakaokuwa na sehemu mbili;
maswali kutoka FIFA na kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
utafanyika saa 4 asubuhi.

Kwa Watanzania wanaotaka kuwa mawakala wa wachezaji wafike TFF ili waweze kupewa
taratibu za mtihani huo ambao ada yake ni dola 50 za Marekani.

Wahusika wa mtihani huo ni wale wanaotaka uwakala kwa mara ya kwanza. Kwa wale
wenye leseni za uwakala wanatakiwa kuziuhisha (renew) kila baada ya miaka
mitano.

Mpaka sasa Tanzania ina mawakala saba wa wachezaji wanaotambuliwa na FIFA.
Mawakala hao ni Ally Mleh wa Manyara Sports Management, Damas Ndumbaro, John
Ndumbaro, Mehdi Remtulla, Ally Saleh, Yusuf Bakhresa na Said Tully.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)