*Villa Squad, JKT Ruvu kukamilisha raundi 21
Na Mwandishi Wetu
MECHI namba 146 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Mtibwa Sugar na Simba iliyochezwa Machi 18 mwaka huu Uwanja wa Jamhuri, Morogoro imeingiza sh. 31,230,000.
Jumla ya watazamaji 10,410 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa kiingilio cha sh. 3,000. Baada ya kuondoa gharama za awali za mchezo na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 4,763,898.31 kila timu ilipata sh. 6,508,230.51, uwanja sh. 2,169,410.17.
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Morogoro (MRFA) sh. 867,764.07, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 2,169,410.17, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,084,705.08, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 216,941.02 na asilimia 10 ya gharama za mechi sh. 2,169,410.17.
Gharama za awali za mechi zilikuwa nauli ya ndani kwa waamuzi sh. 10,000, nauli ya ndani kwa kamishna wa mchezo sh. 10,000. mwamuzi wa akiba sh. 30,000, posho ya kujikimu kwa waamuzi sh. 120,000 na tiketi sh. 2,480,000.
Gharama nyingine ni Jichangie ambayo ni sh. 200 kwa kila tiketi; kila klabu ilipata sh. 728,700 wakati Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Morogoro (MRFA) kilipata sh. 624,600.
Wakati huo huo; mzunguko wa 21 wa Ligi Kuu ya Vodacom unakamilika leo Machi 21 mwaka huu kwa mechi namba 147 kati ya Villa Squad na JKT Ruvu itakayochezwa Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.
Machi 24 mwaka huu kutakuwa na mechi ya ligi hiyo kati ya Moro United na African Lyon. Mechi hiyo namba 149 itafanyika Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.
Mechi za Machi 28 mwaka huu ni Ruvu Shooting Stars itakayocheza na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Mabatini mjini Mlandizi wakati Moro United itakuwa mwenyeji wa Villa Squad katika mechi namba 153 itakayofanyika Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.