Mti wa Kihistoria Waanguka Makumbusho ya Taifa Dar

Sehemu ya tawi la mti wa kihistoria ujulikanao kama Mkuyu uliopo Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni likiwa limedondokea sehemu ya jengo la Makumbusho.

 

MTI mkubwa wa kihistoria aina ya Mkuyu wenye kusadikiwa na miaka zaidi ya mia moja (100) uliopo Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam umekatika tawi kubwa na kuangukia sehemu ya jumba hilo na kuleta madhara kidogo kwenye Jengo hilo.

Mashuhuda wa tukio hilo lililotokea mnamo saa saba mchana walisema hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa wala kupoteza maisha mara baada ya mti huo kuanguka, kwani wakati ukianza kuanguka waliokuwepo karibu na mti huo walisikia sauti kubwa mithili ya mvua kubwa inavuma na kuona tawi linaelekea chini hivyo kutimua mbio kuondoka eneo hilo.

 

Sehemu ya tawi la mti wa kihistoria ujulikanao kama Mkuyu uliopo Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni likiwa limedondokea sehemu ya jengo la Makumbusho hiyo.