Mtera Shooting Yaibuka Mabingwa Lukuvi Cup 2014

waziri Nkamia akimkabidhi zawadi  mchezaji  wa  timu ya MTERA.

waziri Nkamia akimkabidhi zawadi mchezaji wa timu ya MTERA.

Wachezaji  wa  timu ya Mtera wakiendelea  kuumiliki mpira katikafainali ya Lukuvi Cup kata  ya Migoli Mtera

Mabingwa wa Lukuvi Cup timu ya Mtera  wakimiliki mpita
Mchezaji wa  timu ya Home Boys akiwa chini baada ya mchezaji wa  timu ya Mtera kuupiga kichwa  mpira uliokuwa  ukigombewa
Mashabiki  wakifuatilia  mchezo huo
Naibu  waziri Nkamia  akiwa na makombe ya Lukuvi Cup
Uwanja  ukiwa  umezungukwa na mashabiki kabla ya mchezo kuanza
Shangwe  ya ushindi
waziri Nkamia akiwa  na  mchezaji  bora wa  timu  ya mtera Bw.mzambia

Waziri Nkamia  akimkabidhi kombe  kepteni wa Home Boys

Mashabiki  wakifuatulia  zoezi la zawadi
Na MatukiodaimaBlog

MTERA
Shooting yaibuka mabingwa Lukuvi Cup 2014  kwa kata  ya Migoli jimbo la
Isimani baada ya kuifunga timu  pinzani ya Home Boys kwa  jumla ya
magoli 4-1 katika mchezo wa fainali  ulioshuhudiwa na mgeni rasmi naibu
waziri wa habari ,vijana ,utamaduni na michezo Juma Nkamia.

 
Mchezo
huo  uliochezwa  juzi katika uwanja wa Migoli Mtera uliokuwa  na
upinzani  wa hali ya  juu kwa  timu  zote  kutokana na  kushindwa
kuonyeshana  ubabe  dakika  90 za  mchezo kwa  timu hizo kutoka  sare ya
goli 1-1  kabla ya  kumsaka mshindi kwa  mikwaju ya  penati ambayo
iliiwezesha  timu ya Mtera Shooting  kuigagadua (kuifunga) Home Boys
kwa  jumla ya magoli  hayo 4-1 ambayo  yaliiwezesha  kutwaa kombe na
kiteta cha pesa  taslim kiasi cha Tsh milioni 1 kutoka kwa  mbunge  wa
jimbo la Isimani Wiliam Lukuvi ambae ni  waziri wa nchi  ofisi  ya
waziri mkuu sera na uratibu wa bunge.
 
Kbala
ya  dakika  90 za mchezo  kumalizika timu ya Mtera Shooting iliweza
kuwanyanyua mashabiki wake baada ya kujipatia goli la kwanza  dakika ya
86 kwa  mkwaju wa  penati goli lililowekwa  nyavuni na  Mtei Mlimbwa
huku dakika ya  88  Frank Jackson
aliweza  kuisawazishia timu yake ya  Home boys  goli  hilo hivyo timu
hizo  kutoka uwanjani  dakika 90 kwa  bila mbabe  kujulikana.
 
Hali
hiyo iliweza  kupelekea mashabiki  wa kila  timu na  wachezaji  kupigwa
na butwaa ya nani  kutwaa kombe  hilo kabla ya mwamuzi  kutumia njia ya
matuta kumpata  mshindi ambae  alitokana na ujuzi  wa  kugusa  nyavu
za mwenzake.
 
Akikabidhi
zawadi kwa mshindi wa kwanza, wa pili na wa tatu, Naibu Waziri wa
habari, vijana, utamaduni na michezo, Juma Nkamia,ambaye ndiye alikuwa
mgeni rasmi, alisema kuwa vijana wengi Tanzania wanapenda michezo japo
bado kuna tatizo kubwa kwa viongozi wa michezo hususani walimu wa timu
kwa kutokuwa na mafunzo ya ualimu wa timu.
 
Mapema
katibu  wa mbunge  Lukuvi ,Thom Malenga  alisema kuwa lengo la mbunge
Lukuvi  kuanzisha mashindano hayo ni kuweza  kuhamasisha michezo katika
jimbo  hilo na kuwafanya  vijana  kuepukana na matumizi ya madawa ya
kulevya pamoja na mambo mengine ambayo yanaweza  kuwasababishia  kupata
maambukizi ya VVU.
 
Mbali
na  hilo alisem akuwa  kupitia michezo  wananchi  wanakuwa pamoja na
kuondokana na masuala ya itikadi  vya  vyama wakati  wa  kufanya
shughuli za kimaendeleo.
 
Pia
alisema mbali ya mashindano hayo ya ngazi ya kata  pia ameanzisha
mashindano ya ngazi ya tarafa  ambapo  bingwa atazawadiwa Power tilla
kwa  ajili ya kuanzisha vikundi  vya uzalishaji mali katika tarafa.
 
Waziri
Nkamia
akizungumza kabla ya kukabidhi  zawadi kwa  mshindi wa mashindano hayo
alisema kuwa uamuzi  uliofanywa na mbunge Lukuvi katika kuanzisha
michezo ni uamuzi wa kupongezwa kwani mbali ya kutekeleza ilani ya CCM
katika  michezo bado amewawezesha vijana kupata  fursa ya kuonyesha
vipaji vyao ili kupata nafasi ya kuchezea timu kubwa  zaidi .
 
Hivyo
alisema katika  mchezo huo kwa upande  wake amependezwa na kiwango cha
mchezo cha mchezaji wa timu ya Mtera pia alisema  kuwa mbunge  Lukuvi
ametenga zaidi ya Tsh milioni 30 kwa ajili ya mashindano ya soka katika
jimbo  hilo la Isimani na yeye kama waziri mwenye dhamana  ya michezo
amependezwa  zaidi na jitihada  hizo



Mimi  katika  kuunga mkono  jitihada hizi za Lukuvi  nawaahidi kuwa
nitawasiliana na Lukuvi  ili  mabingwa wakacheze na timu yangu jimboni
Kondoa mkoani Dodoma na mchezo mwingine  waje wacheze hapa Mtera hapo
vipi “.
 
Katika
mashindano hayo NKamia alimkabidhi  mshindi wa kwanza kombe na fedha
taslimu shilingi milioni 1 huku  mshindi wa pili akuikabidhiwa  kombe na
shilingi
500,000,mshindi wa tatu akipewa Tsh  250,000 na mchezaji bora  kutoka
timu ya Mtera akipewa Tsh 100,000