Mtendaji Mkuu wa Idara ya Mahakama ateuliwa

Jaji Mkuu Tanzania, Chande Othuman

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete amemteua, Hussein Kattanga kuwa Mtendaji Mkuu wa Idara ya Mahakama kuanzia Julai Mosi, 2012.

Uteuzi wa Kattanga ni sehemu ya utekelezaji wa Muundo Mpya wa Mahakama, na utekelezaji wa Sheria ya Uendeshaji wa Mahakama Namba 4 ya Mwaka 2011. Sheria hii inaanzisha Kada Mpya ya Waendeshaji wa Mahakama, yaani Court of Administrators.

Hadi anateuliwa kushika wadhfa wake wa sasa, Kattanga alikuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).