Mtanzania Auwawa Nchini Kenya, Kamari Yamponza

Mtanzania Auwawa Nchini Kenya, Kamari Yamponza RAIA wa Tanzania ameuawa na umati mjini Nairobi baada ya yeye kudaiwa kuwashambulia na kuwaua watu wawili katika kasino. Watu walioshuhudia tukio hilo walisema mwanamume huyo alikuwa amepoteza takribani Dola 300 akicheza kamari kabla ya tukio hilo. Baada ya kuliwa aliomba kwa msimamizi wa kasino hiyo aruhusiwe kuweka rehani simu yake ili ajaribu kukomboa fedha alizoliwa lakini akakatazwa kwa madai kuwa haikuwa imefikisha thamani ya kuwekwa rehani, walioshuhudia wanasema. Baada ya hapo inadaiwa aliamua kumchoma kisu msimamizi huyo wa kasino iliyopo Mtaa wa Eastleigh. Mlinzi wa kasino hiyo alipojaribu kumsaidia bosi wake naye alichomwa kisu na kumuua. Baadaye alizidiwa nguvu na umati na kuuawa ndipo alipoanza kula kichapo. Polisi walisema mwanamume huyo ambaye ametambuliwa kwa jina la John Barnabas mwenye umri wa miaka 28 inadaiwa anatoka eneo la Rombo, Mkoa wa Kilimanjaro, nchini Tanzania. Taarifa zinadai kijana huyo awali alikuwa akifanya kazi ya ufundi viatu kabla ya kuanza biashara ya uchukuzi wa kutumia pikipiki, maarufu kama bodaboda nchini Kenya. Kabla ya kisa hicho, waliokuwa wakifanya kazi naye walisema alikuwa ameuza pikipiki hiyo ili kupata pesa za kwenda kucheza kamari. -BBC

Mtanzania Auwawa Nchini Kenya, Kamari Yamponza

RAIA wa Tanzania ameuawa na umati mjini Nairobi baada ya yeye kudaiwa kuwashambulia na kuwaua watu wawili katika kasino. Watu walioshuhudia tukio hilo walisema mwanamume huyo alikuwa amepoteza takribani Dola 300 akicheza kamari kabla ya tukio hilo.

Baada ya kuliwa aliomba kwa msimamizi wa kasino hiyo aruhusiwe kuweka rehani simu yake ili ajaribu kukomboa fedha alizoliwa lakini akakatazwa kwa madai kuwa haikuwa imefikisha thamani ya kuwekwa rehani, walioshuhudia wanasema.

Baada ya hapo inadaiwa aliamua kumchoma kisu msimamizi huyo wa kasino iliyopo Mtaa wa Eastleigh. Mlinzi wa kasino hiyo alipojaribu kumsaidia bosi wake naye alichomwa kisu na kumuua. Baadaye alizidiwa nguvu na umati na kuuawa ndipo alipoanza kula kichapo.

Polisi walisema mwanamume huyo ambaye ametambuliwa kwa jina la John Barnabas mwenye umri wa miaka 28 inadaiwa anatoka eneo la Rombo, Mkoa wa Kilimanjaro, nchini Tanzania.

Taarifa zinadai kijana huyo awali alikuwa akifanya kazi ya ufundi viatu kabla ya kuanza biashara ya uchukuzi wa kutumia pikipiki, maarufu kama bodaboda nchini Kenya.

Kabla ya kisa hicho, waliokuwa wakifanya kazi naye walisema alikuwa ameuza pikipiki hiyo ili kupata pesa za kwenda kucheza kamari.
-BBC