Mtandao wa Mashirika Huru ya Kijamii Waandamana Kuwapinga Boko Haram

Baadhi ya wanafunzi wakiandamana kupinga utekaji wa wanafunzi wenzao nchinii Nigeria leo.

Baadhi ya wanafunzi wakiandamana kupinga utekaji wa wanafunzi wenzao nchinii Nigeria leo.

Baadhi ya viongozi wakuu wa Mtandao wa Mashirika Huru ya Kijamii (CSOs) wakipokea maandamano hayo.

Baadhi ya viongozi wakuu wa Mtandao wa Mashirika Huru ya Kijamii (CSOs) wakipokea maandamano hayo.

Viongozi wakuu wanaounda CSOs, wakiwa wameshikana mikono kuonesha umoja wao na kupinga utekaji wa wasichana uliofanyika Nigeria.

Wanaharakati wakiwa wameshikana mikono kuonesha umoja wao baada ya maandamano ya ndani.

Wanaharakati wakiwa wameshikana mikono kuonesha umoja wao baada ya maandamano ya ndani.

Baadhi ya wanafunzi wakiwa wameshika bango katika maandamano ya ndani kupinga vitendo vya kikatili vya kundi la Boko Haram.

Baadhi ya wanafunzi wakiwa wameshika bango katika maandamano ya ndani kupinga vitendo vya kikatili vya kundi la Boko Haram.

MTANDAO wa Mashirika Huru ya Kijamii (CSOs) nchini Tanzania pamoja na baadhi ya wanafunzi wa kike shule kadhaa za Sekondari jijini Dar es Salaam umefanya maandamano kupinga kitendo cha kikatili kilichofanywa na kikundi cha Boko Haram cha nchini Nigeri cha kuwateka wanafunzi wa kike na kuwashikilia.

Maandamano hayo ya ndani yaliyoshirikisha wanaharakati mbalimbali yamefanyika ndani ya viwanja vya TGNP Mtandao eneo la Mabibo jijini Dar es Salaam, ambapo viongozi wa mashirika yanayounda CSOs walipokea maandamano na kusoma barua maalumu yenye ujumbe wa kupinga utekaji uliofanyika na kuishinikiza Serikali ya Nigeria itekeleze matakwa ya watekaji ili wanafunzi waliotekwa waachiwe huru.

Akisoma barua hiyo kwa niaba ya CSOs, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Bi. Lilian Liundi alisema mashirika yao yanaotetea haki za wanawake na watoto yameamua kuungana na mitandao na wanaharakati wengine duniani kote kulaani kitendo cha kinyama cha kuwateka nyara wasichana wanafunzi zaidi ya 200 waliokuwa shuleni nchini Nigeria, tukio lililofanywa na wanamgambo wa kikundi cha Boko Haram.

Baadhi ya viongozi wakuu wa CSOs, kutoka kushoto ni Mkurugenzi TWEWE, Edda Mariki, Mkurugenzi wa WLAC, Theodosia Muhulo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Bi. Lilian Liundi wakizungumza na wanahabari na wanaharakati wengine baada ya maandamano.

“…Kwa pamoja tunakitaka kikundi cha Boko Haram kuwaachia mara moja watoto hao na kuwarudisha haraka majumbani kwao! Kama wanaharakati na watetezi wa haki za wanawake na wasichana tunaitaka serikali ya Nigeria kuchukua hatua zote muhimu zinazotakiwa ili kuokoa maisha ya wasichana hao wasio na hatia, na kuwahakikishia haki yao ya msingi ya kupata elimu na kutembea kwa uhuru bila vitisho,” alisema Bi. Liundi.

Alisema mashirika hayo yametumia maadhimisho ya siku ya kimataifa ya familia ulimwenguni kulaani kitendo hicho cha kikatili na kuitaka Serikali ya Nigeria kuhakikisha inawajibikaji ipasavyo ili kuwarejesha mateka hao mara moja tena wakiwa salama.

“Tunaikumbusha serikali ya Nigeria kuzingatia na kutekeleza tamko la Umoja wa Mataifa la haki za watoto (United Nations Convention on the Rights of the Child (CRC) ambalo liliridhiwa na Tanzania mwaka 1989 na Nigeria mwaka 2003. Mwisho tunatoa wito kwa viongozi wote wa Afrika na jumuia ya kimataifa kuimarisha ulinzi wa wanawake na watoto ili kuhakikisha tukio kama hili halitokei tena mahali pengine,” alisema Liundi akisoma barua maalumu itakayowasilishwa ubalozi wa Nigeria.

CSOs wamelazimika kufanya maandamano hayo ya ndani baada yale ya kutaka kuandamana hadi Ubalozi wa Nigeria kuzuiwa na Jeshi la Polisi kwa sababu kadhaa. Hata hivyo baadhi ya askari polisi walikuwa pembeni mwa viwanja vya TGNP Mtandao katika huku zoezi la maandamano ya ndani likiendelea.

Baadhi ya Mashirika yanayounda CSOs ni pamoja na TAMWA, TGNP Mtandao, WiLDAF, LHRC. Viongozi wakuu walioshiriki maandamano hayo ni pamoja na Mkurugenzi TWEWE, Edda Mariki, Mkurugenzi wa WLAC, Theodosia Muhulo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Bi. Lilian Liundi wakizungumza na wanahabari na wanaharakati wengine baada ya maandamano.
Picha zaidi za matukio ya maandamano hayo baadaye

*Imeandaliwa na www.thehabari.com