Mtandao wa Jumia Tanzania Watoa Ofa kwa Wateja

Meneja wa Jumia Tanzania, Lauritz Elmshauser kulia akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) ofisini kwake.

Meneja wa Jumia Tanzania, Lauritz Elmshauser kulia akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) ofisini kwake.

 

Baadhi ya wanahabari wakiwa katika mkutano na Meneja wa Jumia Tanzania, Lauritz Elmshauser.

Baadhi ya wanahabari wakiwa katika mkutano na Meneja wa Jumia Tanzania, Lauritz Elmshauser.

 

Mkutano huo ukiendelea.

Mkutano huo ukiendelea.

 

MTANDAO unaotoa huduma za mauzo na manunuzi ya bidhaa kupitia intaneti nchini Tanzania ‘Jumia Market-Tanzania’ umetangaza ofa maalumu ya punguzo la bei kwa wateja watakao nunua bidhaa kupitia App ya Jumia. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Meneja wa Jumia Tanzania, Lauritz Elmshauser alisema punguzo hilo ni la shilingi 5,000 kwa mteja yoyote atakayefanya manunuzi kupitia simu yake kwa mtandao wa Jumia.

Alisema mteja atakayefanya manunuzi kwa kutumia App ya Jumia atapunguziwa kiasi hicho cha shilingi 5,000 kwa bidhaa atakayoinunua. Aliwataka wananchi kada mbalimbali kufanya manunuzi kwa kutumia mtandao kwani yanaokoa muda na usalama mkubwa, kuliko mtu kuzunguka akitafuta huduma hizo madukani huku akiwa amesimamisha shughuli nyingine.

Aliongeza kuwa licha ya usalama uliopo mteja huletewa bidhaa yake hadi eneo alipo jambo ambalo linaokoa muda wake wa shughuli nyingine.