Mtalii wa Denmark Abakwa Nchini India

Indian Police badge

Indian Police badge

POLISI nchini India wanachunguza kisa cha mtalii wa kike raia wa Denmark aliyebakwa na genge la watu mjini Delhi. Taarifa zinasema mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 51 alikuwa amepotea njia wakati akirejea hotelini alikokuwa anaishi katikati mwa Mji wa Delhi.

Taarifa zaidi za Polisi zinasema mtalii huyo aliporwa kwa mabavu na kisha kubakwa akishikiwa kisu. Tayari mwanamke huyo ameondoka India Jumatano asubuhi. Pameanza kuwa na umakini kuhusiana na visa vya ubakaji nchini India tangu mwanafunzi aliyefariki mwaka 2012 baada ya kubakwa akiwa kwenye basi mjini Delhi.

Serikali iliweka sheria kali zaidi kuhusu visa vya dhuluma za kingono mwaka jana baada ya maandamano kufanyika kulaani kitendo cha ubakaji. Mwanamke huyo aliambia polisi kuwa aliwaomba wanaume hao kumueleka alikokuwa anaishi baada ya kupotea lakini badala yake wakambaka.

Wanaume hao walimuibia na kisha kumbaka. Mwezi Machi mwaka jana mtalii mmoja raia wa Switzerland alibakwa na genge la wanaume katika Jimbo la Madhya Pradesh. Wanaume sita walifungwa jela maisha kwa kitendo hicho.

-BBC