Mtaka Apata Shavu Shirikisho la Riadha la Dunia

Rais wa Shirikisho la Riadha Duniani (IAAF) Lord Sebastian Coe (kushoto) akipeana mkono na Rais wa Shirikisho la riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka.

Rais wa Shirikisho la Riadha Duniani (IAAF) Lord Sebastian Coe (kushoto) akipeana mkono na Rais wa Shirikisho la riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka.

Mchezo wa Riadha Duniani (IAAF) limemteua Rais wa Shirikisho la Riadha nchini (RT) Anthony Mtaka kuwa miongoni mwa wajumbe wanaounda kundi la ushauri wa mikakati ya mawasiliano la shirikisho hilo.

Sebastian Coe alitangaza uteuzi huo hivi karibuni ambapo wajumbe wengine ni Abrahamson Alan wa Marekani, Rodan Joe Junior

Akizungumza kuhusu uteuzi huo Mtaka ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Simiyu alisema amepokea uteuzi huo kwa furaha kutokana na kuwa ni nafasi ya juu katika sekta maarufu ya michezo katika
ngazi ya kimataifa.

“Nimefurahishwa na uteuzi huu hasa ukizingatia nimeteuliwa nikiwa rais wa shirikisho la riadha mwenye umri mdogo kuliko wote kwa sasa takuwa na fursa ya kujifunza mambo mengi mazuri.”alisema Mtaka.

Alisema uteuzi huo ni faida kubwa kwa maendeleo ya michezo katika taifa letu, hasa kipindi hiki ambapo serikali ya awamu ya tano anapoandaa mkakati wa kuiweka sekta ya michezo
kuwa sehemu kubwa ya ajira.