SERIKALI ya Afrika Kusini imesema kampuni iliyotoa tafsiri kwa lugha za ishara wakati wa ibada ya kumbukumbu kifo cha Nelson Mandela ilidanganya. Imesema kampuni iliyomtoa mtafsiri huyo wa lugha za ishara imekuwa akidanganya kwa miaka mingi huku ikionekana kutoa tafsiri ya kiwango cha chini.
Wataalamu wa lugha za ishara wamesema mtafsiri huyo wa lugha za ishara aliyefanya kazi hiyo, Thamsanqa Dyanty, alikuwa “akitapatapa” wakati wa ibada hiyo siku ya Jumanne.
Hata hivyo Naibu Waziri wa Afrika Kusini, Hendrietta Bogopane – Zulu amesema hakuna suala lolote la kukiuka taratibu za kiusalama wakati mtafsiri huyo alipokuwa akisimama kwani alikuwa na vibali halali. Katika maoni yake mtafsiri huyo anayelalamikiwa yeye amejitetea kuwa alipatwa na ugonjwa wa kuchanganyikiwa akiwa kazini.
Kwa upande wake mmiliki wa kampuni iliyomtoa mtafsiri huyo ametupilia mbali madai ya Naibu waziri Bogopane Zulu. Awali Naibu Waziri huyo aliwaomba radhi jamii ya viziwi kwa kiwango cha chini cha kutafsiri kilichofanywa na Bwana Dyantyi kutoka kampuni ya SA Interpreters.
“Mtafsiri huyo anazungumza lugha ya Xhosa hivyo kiingereza kilikuwa kigumu sana kwake,” alisema Waziri huyo.
-BBC