Mstahiki Meya Jerry Silaa akiingia katika msikiti wa dhehebu la Wahindu kuhudhuria ibada maalum ya kuliombea taifa Amani.
Waendesha Ibada maalum kutoka India katika moja ya hatua za ibada hiyo wakimpa baraka za namna ya pekee Mstahiki Meya Jerry Silaa.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akishiriki kuomba dua na waumini wa dhehebu hilo.
Mstahiki Meya Jerry Silaa katika hatua nyingine ya ibada hiyo akizungushwa ndani ya msikiti huo.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akiwa na Mwenyekitiki wa Jumuiya ya Wahindu Bw. Ramesh Patel (kulia) na Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Bw. Rajesh Mistry.
Pichani Juu na Chini watoto kwa wakubwa wakicheza ngoma za asili ya Hindu kwenye Ibada hiyo.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akioneka kufurahishwa na ngoma hizo.
Pichani Juu na Chini ni Mstahiki Meya akivishwa Ua na vazi la heshima kutawazwa kuwa mmoja wanajumuiya ya Hindu.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akizungumza na wanajumuiya ya Hindu ambapo amewashukuru kwa kumkaribisha kuungana nao katika Ibada hiyo maalum na kuwataka kuendelea kuwa na mshikamano na jamii nyingine pamoja na Serikali.
Mstahiki Meya ametumia fursa hiyo kuwataka wanajamii hiyo pale wanapokwama au kukwazwa kibiashara katika manispaa ya Ilala kwa jambo wanaloona linaweza kutatuliwa wasisite kuwaona viongozi wao na kuwaambia viongozi wao wasisite kumuona yeye moja kwa moja ili watafute ufumbuzi kwa manufaa ya Manispaa na jiji kwa ujumla. Kulia ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Bw. Ramesh Patel.
Igizo lililoonyeshwa baada ya kumalizika kwa Ibada hiyo.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jery Silaa katika picha ya pamoja na wanakikundi cha ngoma za asili ya Hindu.
Picha Juu na Chini ni baadhi ya Waumini wa dhehebu ya Hindu waliohudhuria Ibada Maalum ya kuliombea Taifa Amani.