Mstahiki Meya Manispaa ya Ilala Akizindua Kambi ya Starkey

Mstahiki Meya Jerry Silaa akivishwa Custom made earphones na mmoja wa madaktari bingwa katika kambi hiyo mara baada ya kuzindua huduma hiyo atakayokuwa ikitolewa bure kwa wananchi wenye matatizo ya kusikia.


Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akilakiwa na uongozi wa Starkey alipowasili katika shule ya Buguruni Viziwi kuzindua kambi ya Starkey itakayokuwa inatoa huduma ya uchunguzi, vifaa na matibabu bure kwa wananchi wenye matatizo ya kusikia.

Mstahiki Meya Jerry Silaa akipewa maelezo na mmoja wa wauguzi katika kambi hiyo mara baada ya kuwasili.

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akifanyiwa uchunguzi wa tatizo la kutosikia wakati kuzindua kambi ya Starkey itakayosaidia kutoa huduma na matibabu bure kwa wananchi wenye matatizo ya kusikia iliyopo kwenye shule ya watoto wenye ulemavu wa kusikia (Buguruni viziwi) jijini Dar.

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa jana tarehe 16 April 2013 amezindua kambi ya Starkey ya kusaidia wananchi wenye matatizo ya kusikia iliyofanyika katika shule ya watoto wenye ulemavu wa kusikia (Buguruni viziwi), ambapo wenye magonjwa watatibiwa na wenye kuhitaji vifaa vya kuongezea usikivu watatengenezewa kulingana na size zao na watapewa bureee.

Mstahiki Meya amepima na kwa kuwa ameonekana kutokuwa na tatizo amepata fursa ya kutengenezewa “custom made earphones” wote wenye matatizo mnakaribishwa. Huduma hii ni bureee…

Mstahiki Meya Jerry Silaa akimsalimia mmoja wa watoto waliofika kambini hapo kupatiwa huduma baada ya kuizindua.

Mstahiki Meya Jerry Silaa akipewa maelezo ya namna huduma hiyo itakavyokuwa ikitolewa kwa wagonjwa watakaofika kambini hapo.

Mstahiki Meya Jerry Silaa akibadilishana mawazo na baadhi ya viongozi wa kambi hiyo mara baada ya kuzindua.