Msondo Ngoma Waingia Studio Kutoa Mpya

Msondo Ngoma ikifanya mambo

BENDI Kongwe ya Muziki wa dansi nchini Tanzania ya Msondo Ngoma imeingia Studio kurekodi nyimbo zake mpya zitakazokuwa katika album moja. Akizungumza na waandishi wa habari Msemaji wa Bendi Hiyo, Rajabu Mhamila ‘Super D’ alisema kuwa bendi yake kwa sasa imeingia studio kukamilisha kurekodi nyimbo zao mpya ambazo zinatarajia kuvuta hisia ya wapenzi wa muziki nchini.

Alizitaja nyimbo hizo kuwa ni pamoja na Suluhu uliotungwa na Shabani Dede, Lipi Jema uliotungwa na Baba Kibebe wa Eddo Sanga, Nadhili ya Mapenzi wa Juma Katundu, Kwa momba hakuna Uridhi, Machimbo. Aliongeza kuwa nyimbo zote hizo zikikamilika zitawekwa kwenye albam moja kwa ajili ya kuwapa raha mashabiki wao.

Super D aliongeza kuwa bendi hiyo kwa sasa imesimamisha maonesho yake lakini watakapoanza

sikukuu ya Idi mosi watatoa burudani katika ukumbi wa DDC Kariakoo idi pili watakua TTC

Chang’ombe na idi tatu watavuka bahari kuelekea visiwa vya karafuu na kufanya onesho lao

Zanzibar.

Bondi hiyo kwa sasa inatamba na nyimbo zake mbalimbali wameweka nia ya kukonga mashabiki wa

bendi hiyo kwa kupiga nyimbo mpya na zazamani ili kila mtu apate burudani unajua bendi yetu

kongwe lazima tutoe burudani za aina tofauta aliongeza Super D.

Bendi hiyo iliyopata umarufu mkubwa miaka ya nyuma imewahakikishia wapenzi wake kurudi katika

ubora ule ule kama ilivyokuwa awali.