Msimu wa Nne wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula Waanza

 Eluka Kibona, Meneja Utetezi na Ushawishi wa Oxfam akielezea kwa ufupi juu ya Mchakato mzima wa Shindano la Mama shujaa wa chakula ambalo linalenga kuwawezesha wakina mama kutambulika katika kilimo na kueleza Matakwa yao juu ya kilimo endelevu.

Eluka Kibona, Meneja Utetezi na Ushawishi wa Oxfam akielezea kwa ufupi juu ya Mchakato mzima wa Shindano la Mama shujaa wa chakula ambalo linalenga kuwawezesha wakina mama kutambulika katika kilimo na kueleza Matakwa yao juu ya kilimo endelevu.

Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster akiwashukuru wadau mbalimbali ambao wamefanikisha mchakato mzima wa kuendesha shindano la Mama Shujaa wa
Chakula, Pia Kipekee Amewashukuru wafanyakazi wa Oxfam akiwepo Eluka Kibona na Suhaila Thawer kwa kuwa Mstari wa mbele kufanikisha shindano hilo.
 Baadhi ya washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 wakiwa katika Sherehe ya kukaribishwa hapo jana katika kijiji cha Makumbusho
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Kisalawe Bw. Ellioth Phillemon
akiwakaribisha washiriki wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula Wilayani
Kisalawe.
  Bi. Mwanaidi Hamza ambaye anatoka katika Programu ya Big Result now
akitoa ushuhuda jinsi gani alivyofanikiwa kulingana na Proramu hiyo na
sasa anamaisha mazuri, na kuwasihi wakina mama wasikate tamaa katika
kilimo.
  Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw.
Jackson Samwel akiwapongeza Shirika la Oxfam kupitia kampeni yake ya
Grow kuanzisha shindano la Mama shujaa wa Chakula , kwa kutambua umuhimu
wa ardhi katika kuzalisha chakula, ameshauri akinamama wabadilishane
uzoefu pindi watakapokuwa kambini ili kuja na mbinu mpya za kilimo,
ufugaji na uvuvi.
 Wanao onekana Mbele ni Baadhi ya wenyeji ambao ndio watakuwa wenyeji wa
washiriki wa mama shujaa wa chakula pindi watakapokuwa kijijini.
 Baadhi ya wageni waalikwa katika Sherehe hizo  za kuwakaribisha Washiriki wa shindano la Mama Shujaa wa chakula linalo endeshwa na Shirika la Oxfam katika Kampeni yao ya Grow.