MPIGAPICHA na Mhazini wa Chama cha Wapigapicha za Habari Tanzania (PPAT) , LEAH SAMIKE anawatangazia kifo cha mume wake Bwana HUMPHREY GEORGE LUPENZA aliyekuwa Mkurugenzi Mtedaji wa Lucky Construction Limited, (pichani) kilichotokea leo Saa 10: 55 alfajiri katika Hospitali ya Hindu Mandal Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa matibabu tokea Jumapili.
Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa Marehemu, Kipunguni B -Ukonga Moshi Bar. Jirani na Kanisa la Pentekoste (Kanisa la Mabati). Ukipata taarifa hii mtaarifu na mwenzako. Marehemu ameacha Mke Leah William Samike na watoto 5 ambao ni Maximillian-Samike, Mary -Maria Clara, George, Harrison na Jane-Fatuma. Tuungane na familia ya Marehemu katika kuipa faraja.
Humphrey akiwa na Mkewe Leah Samike siku ya harusi yao mara baada ya kula kiapo chao cha ndoa cha kuishi pamoja milele hadi kifo kitakapowatenganisha.
MUNGU AIWEKE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI AMINA.