Msiba Mzito Arusha, Majonzi Yatawala, Maombolezo Kila Kona…!

Miili ya wanafunzi 32, walimu Wawili na Dereva wao mmoja ikiwa katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha tayari kwa heshima za mwisho.

 

Miili ya wanafunzi 32, walimu Wawili na Dereva wao mmoja ikiwa katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha tayari kwa heshima za mwisho.

 

JIJI la Arusha na viunga vyake leo limezizima kwa manjozi wakati miili ya wanafunzi 32, walimu Wawili na Dereva wao mmoja wote kutoka shule ya Lucky Visent ilipoagwa rasmi kitaifa kabla ya mazishi yao. Hali hiyo ya majonzi na maombolezo imetawala Tanzania nzima tangu kutokea kwa taarifa hizo za kusikitisha zilizomgusa kila mmoja.

Kwa mara ya kwanza idadi kubwa ya mitandao ya kijamii imeridhia kuomboleza vifo hivyo vya wanafunzi 32 pamoja na walimu wao na dereva mmoja vilivyotokea wakiwa safari ya kimasomo. Idadi kubwa ya magrupu ya mitandao ya kijamii hasa wasapu yameomboleza kwa kuweka alama moja wapo za majonzi katika magrupu yao wakikubaliana kuungana kuomboleza msiba huo mkubwa uliolikumba taifa.

Wakati huo huo, MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameongoza mamia ya wananchi wa mkoa wa Arusha na Mikoa ya Jirani katika kuaga miili ya wanafunzi 32, walimu Wawili na pamoja na Dereva Mmoja wa shule ya Lucky Visent katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha waliopata ajali katika eneo la Rhotia wilayani Karatu mkoani Arusha.

Katika hotuba yake kwa wananchi waliojitokeza kwa wingi katika tukio la kuaga miili hiyo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amewahakikishia waombolezaji kuwa Serikali ipo pamoja nao katika kipindi hiki kigumu na chenye majonzi mazito kwa kuondokewa na wapendwa wao.

Amehimiza wananchi kote nchini kuungana katika msiba uliotokea kwa kuwafiriji wafiwa katika kipindi hiki kigumu na kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu wote mahali peponi.

Makamu wa Rais pia ameiagiza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Jeshi la Polisi nchini, walimu, wazazi na walezi wawe makini katika kuhakikisha kuwa sheria za usalama barabarani zinazingatiwa kwa kuchukua hatua stahiki za kulinda watoto hasa wanapotumia vyombo vya moto kwenye shughuli zao za kimasomo.

Amesema hatua hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kuepusha matukio ya ajali ambayo yanaweza kuzuilika kote nchini.

Makamu wa Rais amewataka madereva nchini kuzingatia sheria za usalama barabarani na waache kutumia pombe na dawa za kulevya ili kuepukana na ajali ambazo zinagharimu maisha ya wananchi.

Makamu wa Rais pia amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Kenya Uhuru Kenyatta na Wakenya kwa ujumla kwa kuungana na Wananchi wa Tanzania katika msiba uliotokea.

Katika kuaga miili ya wanafunzi, walimu na dereva katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha, Rais wa Jamhuri ya Kenya Uhuru Kenyatta amewakilishwa na Waziri wa Elimu wa nchi hiyo Fred Matiang’i.

Ibada na Dua ya kuaga miili hiyo, imehudhuriwa na Mawaziri mbalimbali ikiwemo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mohammed Aboud, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene, Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, Viongozi wa vyama vya siasa na Viongozi wa Dini.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan (kushoto) akiwafariji wanafunzi na wanafamilia wa shule ya Lucky Visent katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha kwenye hafla za heshima za mwisho kwa miili ya marehemu.

 

Viongozi mbalimbali wakiongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan wakiwa katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha tayari kwa heshima za mwisho.

 

Viongozi mbalimbali wakiongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan wakiwa katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha tayari kwa heshima za mwisho.

 

Viongozi mbalimbali wakiongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan wakiwa katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha tayari kwa heshima za mwisho.

 

Wananchi mbalimbali wakiwa katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha tayari kwa heshima za mwisho.

 

Miili ya wanafunzi 32, walimu Wawili na Dereva wao mmoja ikiwasili katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha tayari kwa heshima za mwisho.