Mshindi Tuzo ya Soka ya BBC Kutangazwa Leo.

Tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika kwa mwaka inayoandaliwana BBC, Inatarajia kutangazwa leo muda wowote.

Watatu kati ya watano waliopenya katika mchujo walioteuliwa kuwania tuzo hiyo yupo raia wa Algeria Yacine Brahimi Anayekipiga katika kikosi cha FC Porto ya Ureno.
Yacine+Brahimi+aoKJuFCFGjJm
Mwingine ni mchezaji wa klabu ya Swansea ya Uingereza Andre Ayew, ambaye aliiwezesha nchi yake ya Ghana kufanikiwa kutinga katika fainali za michuano ya kombe la mataifaya Afrika.

Mwingine ni Yaya Toure wa timu ya Manchester City na Ivory Coast, ambaye alitwaa tuzo ya mchezaji bora barani mwezi Februari mwaka huu.

Mshambuliaji wa timu ya Gabon na Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang, ambaye amekuwa katiaka ubora wa hari ya juu kwa sasa katika Klabu yake.
images
Hatahivyo, msenegali Sadio Mane ambaye ameingia katika orodha ya mwisho kwa mar aya kwanza baadaya kufanya mambo makubwa akiwa na timu ya Southampton mwaka huu.