Baadhi ya vimwana wanaoshiriki Redds Miss Temeke wakifanya mazoezi kujiandaa na mpambano huo.
KAMBUNI ya BMP waandaaji wa shindano la Redds Miss Temeke jana ilitangaza zawadi kwa mshindi wa taji hilo mwaka huu pamoja na zawadi za washindi wengine. Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Benny Kisaka amesema mshidi wa mwaka huu atajinyakulia sh. milioni mbili, wapili milioni 1.5
“Zawadi pia imeongezwa kwa mshindi wa pili ambaye mwaka jana alipata Sh milioni 1.2 na sasa atapata Sh milioni 1.5 likiwa ongezeko la shilingi laki tatu. Kwa mshindi kwanza ambayo mwaka jana ilikuwa milioni 1.5, mwaka huu Redds Miss Temeke 2011, atazawadiwa kitita cha Shilingi milioni 2 taslim,” alisema Kisaka.
Alisema nyongeza ipo kwa mshindi wa nne na tano kwa kuwa wanaingia katika ya fainali ya Redds Miss Temeke, mwaka jana mshindi wa nne alipata Sh 300,000 na wa tano alinyakulia Sh 400,000.
“Mwaka huu kutokana na udhamini wa kiwango cha juu kutoka TBL na Vodacom pia, washindi hao wa nne na tano kila mmoja atapata Sh. 500,000. Mshindi wa tatu mwaka jana alipata Sh.800,000 Jumamosi Julai 16 mwaka huu atapata Sh milioni 1,” alisema.
Aliwashukuru wadhamini wake wakuu kampuni ya Bia ya TBL kupitia kinywaji chake cha Redds Original sanjari na Vodacom Tanzania kampuni inayoongoza kati ya kampuni za simu za mkononi nchini ambao pia ni wadhamini wakuu wa Miss Tanzania ambako washindi watatu wa Jumamosi watakwenda kushiriki mashindano hayo mwaka huu.
Pia gazeti la Jambo Leo, Saluni ya kisasa iliyopo katikati ya Jiji ya Sally, 88.4 Clouds FM Redio ya watu, Office Direct, 100.5 Times FM, Jambo Tours na Fredito Entertainment.
Katika zawadi hizo ambazo mshindi atamrithi Genevevive Mpangala, ukiondoa zawadi ya kifuta jasho, maeneo mengine yote yameboreshwa ukilinganisha na mwaka jana kwa taji la Temeke Jumamosi, ambapo mwaka jana kifuta jasho kilikuwa ni Sh. 200,000 kila mmoja na kinabaki hivyo.
Wenzetu wa Vodacom wamekuja na mpango kabambe wa kutoa zawadi hizo za pesa kupitia mtandao wa M-Pesa papo hapo ukumbini na watakuwa na mtaalamu wao kuhakikisha zoezi hilo linafanyika katika matarijio yasiyo tatu ili stahiki ya kila mshiriki ipatikane kwa wakati huo.
Shindano hilo lilinogeshwa na kundi la B-Band linaloongozwa na mwanamuziki Banana Zorro, sanjari na baba yake mzazi, Zahir Ally na msanii AT kutoka Zanzibar ambaye ni mtunzi wa nyimbo za Nipigie, Mama Ntilie, Samaki na sasa Vifuu Tundu.
Warembo wengine waliopata kutwaa taji la Miss Temeke na miaka yao kwenye mabano ni Asela Magaka (1996), Miriam Odemba (1997), Ediltruda Kalikawe (1999), Irene Kiwia (2000), Happiness Magasse (2001), Regina Mosha (2002), Sylvia Bahame (2002) na Cecylia Assey (2004).
Wengine ni Jokate Mwegelo (2006), Queen David (2007) na Angela Lubala (2008), Sia Ndaskoi (2009) na Vodacom Miss Tanzania wa sasa, Geneveive Mpangala.