Wito huo ulitolewa na Kaimu Mkurugenzi wa huduma kwa wateja na shughuli za kanda wa Bohari ya Dawa (MSD), Edward Terry wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam katika ukumbi wa wa idara habari maelezo.
“Wasimamizi wa vituo vya afya na hospitali huleta maoteo ya dawa na vifaa tiba kulingana na idadi ya watu walionao kwenye maeneo yao na mara nyingi uangalia magonjwa yanayoshambulia zaidi maeneo hayo hivyo hakutakiwi kuwa na uhaba wa dawa endapo usimamizi mzuri utazingatiwa, alisema Terry.
Akitolea mfano wilaya ya Iramba, Igunga, Bariadi, babati , Arumeru na Sumbawanga kutokuwa na tatizo la dawa ambapo hufuata kanuni na sheria za uagizaji wa dawa kutoka bohari ya dawa pamoja na kutumia vyanzo vingine vya mapato kuongezea bajeti inayotolewa na serikali.
Pamoja na hilo Teryy aliongeza kuwa usimamizi makini wa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ndiyo utakaofanya changamoto ya ukosefu wa dawa kwenye hospitali na vituo kukoma.
“MSD imeboresha huduma na kumpatia mteja taarifa muhuimu zinazomhusu kwa kuziweka wazi taarifa hizo kwenye mtandao ambapo atapata fursa ya kupata taarifa hizo muda wowote.
Alitaja taarifa hizo kuwa ni pamoja na orodha ya dawa na vifaa tiba zilizopo gharani, bei zake na picha za kifaa husika. Taarifa zingine zilizopo kwenye mtandao wa MSD ni pamoja na mgawo wa fedha kwa kila kituo na hospitali uliotolewa na serikali, fomu ya malalamiko na mrejesho.
Terry aliongeza kuwa baadhi ya hospitali na vituo vya afya na wafanyakazi wasio waaminifu ambao wanadiliki kuzichepusha dawa akitolea mfano taarifa ya hivi karibuni katika kituo cha afya cha Kawawa mkoani Mtwara ambapo alikamatwa ofisa wa kituo cha afya akipakia dawa kwenye pikipiki bila maelezo ya sehemu anapozipeleka.
Alisisitiza wananchi na wanahabari kuwa walinzi shirikishi katika utoaji wa taarifa za upotevu wa dawa kwenye vituo vya afya na hospitali ili wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.
“Tunaposambaza dawa kwenye vituo vya afya na hospitali huwa tuna makabidhianao kati ya MSD na kamati ya afya ya eneo husika, hivyo wananchi wanapoambiwa hakuna dawa waonyeshwe fomu ya makabidhiano ya mwisho ya dawa, taarifa ya mgawanyo wa dawa na hati ya maombi ya kuagiza dawa hizo,”alisema Terry huku akiongeza kuwa MSD imeanza kubandika orodha ya dawa zote katika mbao za matangazo ya dawa zote zilizokabidhiwa katika kituo husika.
Pia alizikumbusha hospitali kuwasilisha mahitaji ya dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendnishi vya maabara katika ofisi za msd za kanda Kanda kabla ya Aprili 30 mwaka huu, maombi hayo yaambatinishwe na kivuli cha mpango wa manunuzi kama unavyoonekana katika vitabu vya halmshauri , Council comprehensive Health plan (CCHP), cha ili mahitaji hayo yashughulikiwe kwa wakati. (Imeandaliwa na mtandao wa http://www.habari za jamii.com)