Msanii Mfuga Bundi Aeleza Namna Anavyowapenda Ndege Hao

Kamanda Ras Makunja akiwa mbele ya makazi ya bundi wake udi udi

MSANII na Kiongozi wa kundi la Ngoma Afrika Bend, Kamanda Ras Makunja ameeleza sababu ya kuwapenda ndege aina ya bundi na kuamua kuwafuga nyumbani kwake, nchini Ujerumani. Msanii huyo alisema bundi ni ndege anaowapenda na ndio maana anawafuga. ! Kwa nini?

Anasema bundi wake ni wakimya na si wakorofi. Baada ya bendi yake kufanikiwa kujichukulia tuzo ya kimataifa ya bendi bora ya kiafrika barani Ulaya, mkuu wa kikosi kazi cha Ngoma Africa Band aka FFU, Kamanda Ras Makunja amekutwa akicheza na bundi wake katika maskani yake ‘Anunnaki Empire’ na alipoulizwa ni kwa nini anawapenda bundi hao, alisema.

“…Bundi ni ndege wapole na hawana ukorofi wala kilele na ukilinganisha na ndege kama kasuku ambao ni ndege wenye kelele,” alisema Kamanda.