Msanii Ebrahim Makunja Ahojiwa na Offener TV

Msanii Ebrahim Makunja Ahojiwa na Offener TV

Kamanda Ras Makunja akihojiwa na Offener Channel TV ya Ujerumani

Kamanda Ras Makunja akihojiwa na Offener Channel TV ya Ujerumani

Kamanda Ras Makunja akihojiwa na Offener Channel TV ya Ujerumani

Kamanda Ras Makunja akihojiwa na Offener Channel TV ya Ujerumani

Kamanda Ras Makunja wa FFU ughaibuni alipomaliza kuhojiwa

Kamanda Ras Makunja wa FFU ughaibuni alipomaliza kuhojiwa

MWANAMUZIKI Ebrahim Makunja a.k.a Kamanda Ras Makunja kiongozi mwanzilishi wa bendi maarufu Ngoma Africa almaharufu FFU-Ughaibuni ya Ujerumani, juzi alifanya mahojiano na kituo cha TV cha Offener Channel ya Ujerumani.

Mwongozaji wa kipindi katika mahojiano hayo, Fischer alimkutanisha msanii huyo pia na wataalam na wadau wa muziki wa kimataifa. Akikaribishwa katika kipindi hicho mwanamuziki Ras Makunja ametajwa kuwa jamii ya ujerumani inauthamini na kuukubali mchango wake wa kutumia muziki katika
kutokomeza ubaguzi.

Historia imemtaja Kamanda Ras Makunja na kikosi kazi Ngoma Africa band kuwa mwaka 1993 alikubali kuzunguka Ujerumani yote akifanya maonesho ya “WE ARE ONE” kampeni iliofanikiwa kuwaunganisha wageni na wenyeji kazi ambayo anasema licha ya kuwa ngumu lakini ilifanikiwa.

Msanii huyo alielezea siri ya mafanikio ya Ngoma Africa ambayo ipo hai zaidi ya miaka 26 huku inadumu na kuendelea kuwanasa washabiki kwa wingi. Kamanda Ras Makunja akijibu baadhi ya maswali alionekana si wakutaka kuweka hadharani kila mbinu, lakini alisema kuwa muziki unachezeka lakini pamoja na kuchezeka.

Aliongeza kuwa wanamuziki wa bendi ya Ngoma Africa band ni watumishi wa washabiki na wadau wa muziki kwa maana hii bendi inamilikiwa na washabiki na wadau ambao wao ndio wanayoitangaza. Sisi tuna vyombo vya muziki tu. Mimi naongoza bendi tu lakini wamiliki ni washabiki na wapenzi wa Ngoma Africa band, bandi hii ni sauti ya umma wa kimataifa pia ni sauti ya wasio sikika “Voice of speachless” ambayo inasikika kimataifa Ras Makunja alisema.

Kama kawaida yake Kamanda Ras Makunja bila kujisihau wapi anatoka yaani mtanzania aliyekunywa maji ya bendera! alipoulizwa juu ya vipaji vya wafrika? Kamanda Ras Makunja moja kwa moja aliwaomba wadau na mapromota wa kimataifa kuwapa nafasi kubwa wasanii waliopo Tanzania kuja kushiriki maonesho ya kimataifa.

Ras Makunja aliwaomba na kuwashawishi maporomota na wadau hao kuwa nchi ya Tanzania ina utajiri wa maelfu ya wasanii wenye vipaji vya ajabu wakiwemo wanamuziki, watengenezaji wasanaa za mikono wanawake kwa wanaume, wacheza maigizo, sarakasi, wachoraji, nendeni Tanzania mkaonane nao, wapeni nafasi wasanii hawa muone jinsi watakavyo kuja kufanya sanaa ambazo hapa ulaya ni adimu.

Ninawaombeni nendeni Tanzania na mkitaka msaada wangu wa kuwaelekeza mimi nipo Tayari – Kamanda Ras Makunja alimalizia kwa kuwaomba wadau na maporomota. Kamanda huyu wa Ngoma Africa Band Ras Makunja alionekana kutumia fulsa kwa kuwapigania wasanii wa nyumbani ili wapate nafasi zaidi ya kimataifa.

Nje ya uringo alipoulizwa mbona ameifagilia Tanzania sana na swali lilikuwa wasanii wa Afrika, Makunja alijibu kwa mkato heti hata Umoja wa mataifa kila nchi ina balozi wake na akatimua zake.